Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

7. Asmir Begovic- sekunde 13

Huyu ni kipa. Ndiyo, kipa anayedakia Bournemouth kwa sasa na kipindi hicho alikuwa kwenye kikosi cha Stoke City. Kitu ambacho kinachovutia hapa ni kwamba humtarajii kipa kufunga bao katika ndani ya mchezo wa muvu, zaidi ya labda kuwa mpira wa adhabu. Mwaka 2013, aliokoa kwa kupiga mpira mrefu ambao ulikwenda kumshinda kipa wa Southampton, Artur Boruc na kutinga wavuni, sekunde ya 13 tu ya mchezo. Lilikuwa bao la mita 91.9.
 
6.Chris Sutton- sekunde 13

Mwaka 1995, Alan Shearer alikuwa akiichezea Blackburn Rovers na pale mbele kwenye fowadi alikuwa akishirikiana na staa Chris Sutton. Walibeba ubingwa wa Ligi Kuu England mwaka huu. Lakini, siku ambayo walicheza na Everton, ile refa anapuliza kipyenga chake tu, sekunde chache tu tayari ilikuwa 1-0, Sutton akifunga kwenye sekunde ya 13 tu huko Goodison Park. Rovers ilishinda 2-1.
 
5.Dwight Yorke- sekunde 13

Mwaka 1995, Dwight Yorke alikuwa hazuiliki uwanjani, alichokuwa akikitaka yeye ni kufunga tu. Kipindi hicho akiwa kwenye kikosi cha Aston Villa, Yorke alifunga ndani ya sekunde 13 tu katika mechi dhidi ya Coventry City. Lilikuwa bao la kwanza kwa Aston Villa katika siku hiyo ambapo ilikuwa tishio uwanjani na kushinda 3-0. Manchester United ikamuona Yorke na kwenda kumsajili
 
4.Mark Viduka- sekunde 11

Mark Viduka, mmoja kati ya mafundi wa mpira waliopata kutokea kwenye Ligi Kuu England. Mwaka 2001, akiwa kwenye kikosi cha Leeds United, straika Mark Viduka aliwaduwaza mabeki wa Charlton Athletics kwa kufunga bonge la bao katika sekunde ya 11 ya mchezo. Staa huyo wa zamani wa Australia aliuwahi mpira wa Alan Smith na siku hiyo Leeds iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
 
3.Christian Eriksen- sekunde 11

Januari 31 mwaka huu, kiungo fundi wa mpira wa Tottenham Hotspur, Christian Eriksen aliwashtua Manchester United kwa bao la mapema sana walipokwenda Wembley. Eriksen alifunga katika sekunde ya 11 tu. Baadaye, beki wa Man United, Phil Jones alijifunga na kuwafanya Spurs kuongoza kwa mabao 2-0 na kilikuwa kipigo kwa Man United na hapo kasi yote ya kuifukizia Manchester City ilikata.
 
2.Alan Shearer- sekunde 10

Gwiji wa Newcastle United, Alan Shearer hakuna ubishi ni mmoja kati ya washambuliaji mahiri kabisa kuwahi kutokea kwenye Ligi Kuu England. Mwaka 2003, Man City ikwenda iliifuata Newcastle uwanjani St.James Park na kilichowakuta huko wenyewe wanakijua. Walichapwa 2-0, lakini kilichovutia ni bao la mapema zaidi ya Shearer alilofunga katika sekunde ya 10 ya mchezo.
 
1.Ledley King- sekunde 9

Beki wa kati wa zamani wa Tottenham Hotspur, Ledley King ndiye anayeendelea kushikilia rekodi ya kufunga bao la haraka zaidi kwenye historia ya Ligi Kuu England. Beki huyo aliamua kupiga shuti katika sekunde ya 9 tu na mpira huo ulikwenda moja kwa moja wavuni. Hiyo ilikuwa kwenye mechi dhidi ya Bradford iliyomalizika kwa sare ya 3-3 mwaka 2000.
 
ARSENE Wenger ameamua kuondoka Arsenal baada ya kuhudumu kwa miaka 22. Anaondoka akiwa bado na kandarasi ya mwaka mmoja, kwa vile alisaini mkataba mpya wa miaka miwili mwaka jana.

Ni uamuzi uliokuja baada ya malalamiko mengi kutoka kwa washabiki, baadhi wakitaka aachie ngazi tangu mwaka juzi, timu ilipoanza kufanya vibaya.
 
Anaondoka baada ya jitihada mbalimbali za mashabiki, ikiwa ni pamoja na maandamano, kuweka mabango ya ‘Wenger Out’ na ndege kupita juu ya dimba lao zikiacha ujumbe huo huo.

Hata hivyo, kubwa na la mwisho ni mashabiki, hasa wale wakubwa wanaonunua tiketi za msimu mzima kugoma kwenda uwanjani Emirates na viti vingi kubaki wazi.
 
Ni kweli amekaa muda mrefu na hakuna ubishi ni ngumu kufikiria mtu mpya kwenye nafasi yake pale kwenye benchi la ufundi. Alizoeleka sana hapo, maana miaka 22 si muda mfupi na baadhi ya mashabiki wa Arsenal hawakuwa wamezaliwa alipoanza kuiongoza klabu hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…