Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

LIGI Kuu England bingwa ndo hivyo keshapatikana, Manchester City. Man City wametangaza ubingwa wiki iliyopita baada ya Manchester United kukutana na kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa West Brom, kipindi ambacho kimewafanya hata washinde mechi zote wasingeweza kufikia pointi za wakali hao wanaonolewa na Pep Guardiola.
 
.
20180424_223335.jpg
 
Vita nyingine ni ile ya kujinusuru na balaa la kushuka daraja. Lakini, kushinda vita hizo unahitaji kushinda mechi na kushinda mechi unahitaji kufunga mara nyingi kwenye mechi kuliko mpinzani wako. Jambo hilo limefanya kupatikana wakali wa kupiga nyingi kwenye mechi moja kwenye Ligi Kuu England msimu huu.
 
Hawa hapa wakali waliofunga mara tatu katika mechi moja ya ligi msimu huu, yaani hat-trick na kwa taarifa yako, wapo wachezaji saba tu waliofanya hivyo kwa msimu huu matata. Kitu kinachovutia, mastraika walionaswa kwa pesa nyingi huko Arsenal, Alexandre Lacazette na huko Man United, Romelu Lukaku, hawapo. Hawahusiki.
 
7. Callum Wilson- Hat-trick 1

Fowadi huyo wa Bournemouth, Callum Wilson Jumatano iliyopita aliwapa wakati mgumu sana mabeki wa Man United, Phil Jones na Chris Smalling, licha ya kwamba hakufanikiwa kutikisa nyavu siku hiyo na Man United ilishinda 2-0, shukrani kwa mabao ya Smalling na Romelu Lukaku. Lakini, Novemba 18 mwaka jana, kwenye mechi dhidi ya Huddersfield, Wilson alipiga hat-trick wakati Cherries iliposhinda 4-0 kwenye Uwanja wa Vitality.
 
Baada ya kutua tu kwenye kikosi hicho cha Chelsea, Morata alihitaji mwezi mmoja tu kupiga bao tatu katika mechi moja, ambapo alifanya hivyo Septemba 23 mwaka jana kwenye mechi dhidi ya Stoke City. Morata alifunga bao la kwanza dakika ya pili yay a mchezo na bao lake la tatu alifunga kwenye dakika 82 kukisaidia kikosi hicho cha Antonio Conte kushinda 4-0 ugenini.
 
5. Aaron Ramsey- Hat-trick 1

Kiungo mchezeshaji wa Arsenal, Aaron Ramsey alikuwa moto kweli kweli, Februari 3, mwaka huu kwenye mechi dhidi ya Everton. Staa huyo wa kimataifa wa Wales alipiga hat-trick matata ndani ya dakika 68 kuisaidia Arsenal kushinda 5-1 huko Emirates.
 
Back
Top Bottom