Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

4. Wayne Rooney- Hat-trick 1

Fowadi wa Everton, Wayne Rooney naye ni moja kati ya wale spesho waliopiga hat-trick kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Staa huyo wa zamani wa Man United alifunga mabao matatu kwenye mechi moja wakati Everton ilipocheza na West Ham
 
Mechi hiyo ilipigwa Novemba 29 mwaka jana uwanjani Goodison Park. Katika mechi hiyo, Rooney alifunga kwa staili kubwa ikiwamo bao lake alilofunga akiwa katikati ya uwanja. Bao hilo liliwafanya mashabiki uwanja mzima kusimama kumshangilia na hakika lilishinda tuzo ya bao bora la mwezi Novemba.
 
3. Mohamed Salah- Hat-trick 1

Kwa msimu huu, kwenye Ligi Kuu England, staa wa Liverpool, Mohamed Salah ndiye kinara wa mabao akiwa ametupia wavuni mara 31 na hakika Kiatu cha Dhahabu cha kwenye ligi hiyo kinamhusu msimu huu. Lakini, katika mabao yote hayo, Salah alifunga mara moja tu mabao matatu katika mechi moja ya ligi na hiyo ilikuwa Machi 17 mwaka huu, wakati Liverpool ilipokipiga na Watford
 
2. Harry Kane- Hat-trick 2

Straika wa Tottenham Hotspur, Harry Kane amekuwa akimfukuzia Mohamed Salah kwenye mbio za Kiatu cha Dhahabu, lakini kwa hali ilivyo kwa sasa, mbio hizo zinaonekana kuelekea kumshinda. Kwa sasa amefunga mabao 26, matano nyuma ya mpinzani wake huyo.
 
Lakini, kwa msimu huu Kane amekuwa kwenye ile orodha ya watu spesho waliopiga hat-trick Ligi Kuu England, Mwingereza huyo alifanya hivyo mara mbili katika mechi mfululizo, dhidi ya Burnley, alifunga mabao yote kwenye mechi hiyo na nyingine ni ushindi wa 5-2 dhidi ya Southampton uwanjani Wembley.
 
Back
Top Bottom