Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20180426-WA0035.jpg
 
Mama wa mwanamuziki Lady Jay Dee, Martha Mbibo amefariki dunia leo asubuhi nyumbani kwake Kiwalani, jijini Dar es Salaam baada ya kuugua saratani ya kibofu.

Akizungumza na MCL Digital, msaidizi wa mwanamuziki Lady Jay Dee, Lucy Mosha anasema msiba upo nyumbani kwa wazazi wa Lady Jay Dee eneo la Kiwalani.

“Mama Mbibo amefariki dunia saa moja asubuhi akiwa nyumbani kwake Kiwalani, taratibu za mazishi zinaendelea na tukipata ratiba kamili tutatoa,” anasema Lucy.

Anasema hali ya Mama Mbibo haikuwa mbaya kwamba awali alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na baadaye kuruhusiwa.

“Alikuwa nyumbani na hospitali alikuwa akipelekwa mara moja moja kwa uchunguzi zaidi,” alifafanua.
 
Back
Top Bottom