A. Kubadilisha maisha na kungoja
Hii ndiyo njia inayopendekezwa kwa wanaume ambao wana dalili kidogo ambazo haziwasumbui.Hata hivyo,haimaanishi kukaa tu bila kufanya chochote.Wakati mgonjwa anangoja,anahitajika kubadili jinsi anavyoishi ili kupunguza dalili zilizopo,na pia kumwona daktari kila mara(walao mara moja kwa mwaka) ili kujua kama dalili zinapungua au zinazidi.
Badili mazoea ya kukojoa na kutumia vinywaji.Kojoa mara kwa mara,usizuie mkojo,kojoa mara tu haja ijapo.Kojoa kwa vipindi viwili, yaani kwanza kojoa kama kawaida, ngoja kidogo na ujaribu kukojoa tena papohapo,usijilazimishe kukojoa.Usinywe pombe wala kahawa jioni.Hivi viwili hulegeza kibofu na kufanya figo kitengeneze mkojo na hivyo basi kukojoa zaidi usiku.Usinywe maji mengi sana.Usizidi lita tatu kwa siku.Usinywe maji mengi mara moja bali unywe kidogo kidogo siku nzima/mchana wote.Punguza vinywaji unapoenda kulala au unapoenda kwenye shughuli nje.Usinunue dawa za homa dukani.Hizi huzidisha dalili na mkojo kutotoka.Badilisha wakati unapokunywa dawa za kukojoza.Jichunge na baridi, weka mwili wako na joto na fanya mazoezi.
Kutokufanya mazoezi huzidisha dalili.
Nb:Tezi dume lililovimba na ambalo linaleta dalili ndogo ndogo linaweza kuangaliwa kwa uangalifu na kwa kubadilisha mfumo wa maisha bila ya kuchukua hatua yoyote ya kidaktari.