Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

. Matibabu ya dawa
Dawa ndizo hutumika na hupendekezwa mara nyingi katika kukabiliana na dalili zenye ukali kiasi.Dawa hupunguza dalili kwa kiasi kikubwa kwa wagonjwa wengi.Kuna aina mbili za dawa, za kulegeza misuli ya kibofu,na za kupunguza ukubwa wa tezi dume.
 
Dawa za kulegeza misuli
Hizi hulegeza misuli ndani na nje ya tezi dume, Hupunguza kizuizi cha mkojo na kuwezesha mkojo kutoka kwa urahisi zaidi. Dawa hizi zinaweza kusababisha kizunguzungu, kichwa kuuma na kuhisi uchovu.Dawa hizi ni kama famsulosin, alfuzosin,terazosin na doxazosin
 
Dawa za kupunguza tezi dume
Hizi hupunguza ukubwa,kuongeza mkojo unaotoka na pia kupunguza dalili.Hazifanyi kazi haraka kama zile za kulegeza misuli.Nafuu hupatikana baada ya kuzitumia kwa kama miezi sita.Huwa bora kwa walio na dalili kali.Matatizo ya dawa hizi ni kukosa ashiki ya kufanya mapenzi na hata kupunguza nguvu ya uume.
 
C. Njia ya upasuaji
Njia hii hupendekezwa kwa watu wafuatao:

Dalili kali ambazo hazisikii dawa.
Mkojo kuziba ghafla.
Maambukizo ya njia ya mkojo ya mara kwa mara.
Damu kwenye mkojo.Figo kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya shida ya tezi dume.
Mawe ya kibofu pamoja na tezi dume iliyopanuka.kuongezeka kwa mkojo unaobaki baada ya kukojoa.
Upasuaji umegawanyika katika aina mbili kukatwa au kuchomwa.
 
. Kukatwa sehemu /kipande cha tezi dume

Hii ndiyo njia ambayo kwa kawaida hutumiwa na huwa nzuri kuliko dawa.Husaidia wagonjwa wengi, asilimia themanini na tano hadi tisiini. Husaidia kwa muda mrefu. Daktari hukata sehemu iliyoziba kwenye njia ya mkojo.Ngozi haikatwi wala kushonwa, lakini mgonjwa lazima alazwe hospitalini kwa operesheni hii.
 
Kabla ya upasuajiNi vizuri kuhakikisha mgonjwa yu katika hali nzuri kimwili.

Dalili kali za kuvimba kwa tezi dume, mkojo kufunga, maambukizi yanayojirudiarudia ya mfumo wa mkojo, na figo kushindwa/kufeli ni dalili zinazohashiria umuhimu wa upasuaji.

Mgonjwa asivute sigara ili kuzuia maambukizo ya kifua ambayo huchelewesha kupona.Mgonjwa anashauriwa asiendelee kutumia dawa zinazofanya damu nyepesi kama vile aspirin,warfavin au clopidogrel.
 
Dawa za kupunguza tezi dume
Hizi hupunguza ukubwa,kuongeza mkojo unaotoka na pia kupunguza dalili.Hazifanyi kazi haraka kama zile za kulegeza misuli.Nafuu hupatikana baada ya kuzitumia kwa kama miezi sita.Huwa bora kwa walio na dalili kali.Matatizo ya dawa hizi ni kukosa ashiki ya kufanya mapenzi na hata kupunguza nguvu ya uume.
Ina maana nguvu za kiume ni mhimu sana Carba?
 
UpasuajiHuchukua kati ya dakika sitini hadi tisini.
Mgonjwa hudungwa sindano ya nusukaputi na hupatiwa dawa za kuzuia maambukizo.
Wakati wa upasuaji,kifaa maalumu (resectoscope) huingizwa kwenye njia ya mkojo kupitia kwenye uume.
Kifaa hiki huwa kina mwanga na kamera ya kupiga picha, waya ya kukata sehemu ya tezi na pia kuziba mishipa ya damu, na njia inayopeleka maji ya kusafisha kwenye kibofu.
Sehemu inayokatwa hutumwa kwenye maabara ili ichunguzwe iwapo ina chembe chembe za saratani.
 
Baada ya upasuaji

Mgonjwa hukaa hospitalini kwa siku mbili hadi tatu baada ya upasuaji.
Baada ya upasuaji katheta au tyubu kubwa huingizwa kwenye njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.
Maji maalum husukumwa hadi kwenye kibofu na kutolewa kwa mfululizo kwa saa kumi na mbili hadi ishirini na nne.
Maji haya huwa ni ya kutoa damu au damu iliyoganda baada ya upasuaji.
Mkojo ukionekana safi bila damu yoyote, basi katheta hutolewa.
 
Kunywa maji mengi kusafisha kibofu.
Zuia kwenda choo na hasa choo kigumu kwani huzidisha kutokwa na damu.
Ukifunga choo tumia dawa ya kuharisha.
Usitumie dawa za kufanya damu kuwa nyepesi bila ushauri wa daktari.
Usifanye kazi ngumu kabla ya wiki nne hadi sita.
Usifanye kitendo cha ndoa kabla ya wiki nne hadi sita.
Usinywe pombe, kahawa wala vyakula vyenye viungo vikali.
 
Matatizo yanayoweza kujitokeza

Matatizo yanayoweza kutokea ni kutokwa na damu au maambukizo.
Pia matatizo mengine ya kawaida yanayotokana na upasuaji.
Matatizo ya baadaye ni njia ya mkojo kuwa nyembamba, kukosa nguvu ya kufanya mapenzi au manii kurudi kwenye kibofu.
Hali hii ya manii ya mwanamme kurudi nyuna kwenye kibofu hutokea kwa wagonjwa wengi.
Hutokea kwa takriban asilimia 70% ya wagonjwa. Lakini huwa haitatizi uwezo wa kufanya mapenzi lakini humfanya mwanamme gumba, yaani hawezi kuzaa.
Hali ambazo huenda zikasababisha matatizo zaidi ni kama vile uzito mkubwa, uvutaji wa sigara, pombe, kukosa lishe bora au ugonjwa wa kisukari.

Nb;Muone daktari iwapo:Unashindwa kukojoa.Maumivu makali ambayo hayatulizwi kwa dawa.

TURP hufanywa kwa kupiga sindano mgongoni. Mgonjwa hapotezi fahamu na haitaji kukaa kwa muda mrefu hosipitalini.

Kutokwa na damu yenye madonge makubwa iliyoganda, ambayo yanaweza kuziba katheta.
Dalili za maambukizo kama homa, baridi au kutetemeka.
Upasuaji wa kibofu ndiyo njia bora zaidi ya kutibu tezi kibofu kilichotanuka.
Upasuaji hufanywa kwa kutumia nusu kaputi iwekwayo mgongoni.
Hii upunguza siku za kukaa hospitalini.
Manii/shahawa kuingia kwenye kibofu ni tatizo la upasuaji na kumfanya mgonjwa asizae.

2. Njia ya tezi kibofu kupasuliwa

Njia hii huwa nzuri kwa wanaume wenye tezi kibofu ndogo au afya upasuaji wa tezi dume kupitia njia ya mkojo (tupi).

Njia hii ni kama zile ambapo tezi inapunguzwa kwa kukatwa lakini badala ya sehemu kutolewa, mikato mirefu yenye kina hupasuliwa kwenye tezi dume.Mikato hii hupanua njia ya mkojo na kuwezesha mkojo kutoka kwa urahisi.

Faida za upasuaji huu ni pamoja na kupoteza damu kidogo, matatizo yanayo ambatana na upasuaji huwa kidogo, muda mfupi hospitalini na kupona haraka.Pia ile hatari ya mkojo au manii kurudi nyuma huwa nadra.Kasoro za njia hii ni kutofaulu katika kumaliza tatizo kabisa,na pengine tatizo kurudi tena.Wakati mwingi wagonjwa hurudia kutibiwa baadaye kwa ile njia ya kupunguza tezi dume kwa kukata sehemu yake. Upasuaji huu (TUIP) si njia mwafaka kwa wagonjwa wenye tezi dume kubwa.

3. Upasuaji

Hapa mgonjwa hufunguliwa tumbo na tezi dume hutolewa.Siku hizi

TUIP ni njia mbadala ya TURP kwa wanaume wenye tezi dume dogo na ambao upasuaji wa TURP si mzuri kwao.

njia hii haitumiki sana kwa sababu kuna njia nyingine nyepesi ambazo zimegunduliwa.Njia hii hutumika tu kwa wazee ambao tezi zao zimekuwa kubwa sana au wenye matatizo mengine yanayohitaji upasuaji huu.

Njia zisizo za upasuaji

Njia hizi huwa hazina maumivu mengi kwa sababu ya uvumbuzi wa kitekenolojia. Njia hizi hulenga kutibu tatizo la tezi dume kwa kupanuka kwa njia rahisi iwezekanavyo:Njia hizi kwa kawaida hutumia joto,miale,na nguvu za umeme kupunguza tezi dume.Njia hizi zote hufanywa kwa kupitia njia ya mkojo ya yurethra iliyo kwenye uume. Faida za njia hizi nyepesi huwa ni :muda mfupi wa kukaa hospitalini,dawa kiasi ya ganzi (Anaesthesia),hatari na matatizo kidogo kuliko upasuaji na pia kupona haraka.

Kasoro zake ni pamoja na uwezekano wa ugonjwa kurudi baada ya muda fulani na hivyo mgonjwa kuhitaji upasuaji, mara nyingi baada ya miaka mitano hadi kumi.Kwa sababu sehemu ya tezi haitolewi,uchunguzi wa magonjwa mengine kama vile saratani haufanywi kwa hivyo usalama wake si kama ule wa sehemu ya tezi kutolewa.Shida nyingine ni kuwa njia hizi zisizo za upasuaji hazipatikani kwenye nchi zinazoendelea kwa urahisi na pia huwa ghali.Njia nyingine zisizo za upasuaji zinazotumika kutibu tezi dume iliyotanuka huwa ni;

Kuchoma kwa mawimbi ya sitima.Kumomonyoa kwa sindano.Kuchoma kwa maji moto.Kuwekwa springi au koili.Kuchomwa kwa miale.

1. Kuchomwa kwa joto la wimbi la maikro : sehemu ya tezi iliyoziba njia ya mkojo huchomwa/huunguzwa.

Faida za MIT: Hatari ni chache na hulazwa kwa muda mfupi hosipitalini.

2. Kumomonyoa kwa kutumia sindano ya umeme :kwa kutumia nguvu za umeme, sehemu ya tezi iliyoziba mtiririko wa mkojo hugadishwa na kuondolewa.

3. Kuchomwa kwa maji moto : Maji moto husababisha sehemu ya tezi ambayo haitakikani kuganda na kuondolewa.

4. Kuwekwa springi au koili : Springi au koili huwekwa katika sehemu ya yurethra iliyofinywa ndani ya tezi ili kuiweka wazi na kurahisisha mkojo kupita.

5. Kuchomwa kwa miale : sehemu iliyoziba njia ya mkojo humalizwa kwa kuchomwa.

Je,mgonjwa wa tezi dume lililotanuka anafaa kumwona tena daktari lini?Akishindwa kukojoa kabisa.Kuwashwa au uchungu akikojoa, mkojo wenye harufu mbaya, homa na kuhisi baridi.Damu kwenye mkojo.Kushindwa kuzuia mkojo na nguo za ndani kulowa mkojo.

Kuweka bangili ( stent)kwenye tezi dume ni matibabu salama na yanayofaa hasa wakati matibabu ya kawaida hayakufaa na upasuaji haupendekezwi.


 
Back
Top Bottom