Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Matapeli hao wamekuwa wakiwatumia ujumbe wazazi kuwa watoto wao ni wagonjwa na wamepelekwa hospitali hivyo, kuomba fedha za haraka kusaidia kuharakisha matibabu.

Na ili kukuaminisha, matapeli hao hujifanya ni walimu wa mtoto wako na kutoa taarifa zinazoweza kukuaminisha kwa haraka kuwa kuna tatizo la kweli. Zaidi ya hayo, husisitiza kuwa hali ya ugonjwa wa mtoto wako ni mbaya, hivyo kuhitaji msaada wa fedha ili kuokoa maisha yake.
 
Habari ndugu mimi ni mwalimu, mtoto anaumwa hapa shuleni tuwasiliane haraka,” unasema ujumbe wa tapeli mmoja uliotumwa kwa mzazi ambaye mwanaye anasoma shule moja wilayani Temeke.

Akizungumza na Mwananchi, mzazi huyo, aliyeomba jina lake lihifadhiwe, alisema Aprili 24 saa 5:04 asubuhi alipokea ujumbe huo mfupi wa simu ukimtaarifu kuwa mtoto wake anayesoma kidato cha kwanza, anaumwa.
 
Baada ya kuusoma aliamua kupiga namba iliyomtumia ujumbe huo ili apate taarifa zaidi.

Alisema alipompigia simu mtu huyo alimweleza kuwa mtoto wake anaumwa na hali yake ni mbaya na kwamba wapo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), hivyo afanye awezalo aende hospitalini haraka.
 
Wakati nikipigiwa simu, nilikuwa na watu wakanishauri nifanye mawasiliano na mwalimu wa mtoto wangu kama nina namba zake,” alisema.

“Bahati nzuri nilikuwa na mawasiliano na mwalimu wa darasa nikampigia. Akaniambia mtoto ni mzima na yupo naye jirani.”
 
Mzazi huyo alisema taarifa hiyo iliushtua uongozi wa shule ulioamua kufuatilia suala hilo kwa kufanya mawasiliano na mtu aliyempigia simu mzazi na kujitambulisha kuwa ni mwalimu.

Alisema mratibu wa shule alimpigia simu mtu huyo akijitambulisha kuwa ni mzazi na kuhoji mtoto huyo anaitwa nani ili apate uhakika kama ni wake.
 
Mtu huyo alitaja majina matatu ya mtoto huyo na kueleza kuwa anaugua UTI kali, hivyo zinahitajika Sh68,500 kwa ajili ya vipimo.

Mwalimu aliyekuwapo wakati wa mawasiliano hayo alisema yalikatika ghafla baada ya mratibu wa shule kumjulisha tapeli kuwa mtoto yupo shuleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…