DaaaaMatatizo ya tezi dume iliyotanuka
Tezi dume ikitanuka sana huleta matatizo mengi kwa wagonjwa wengine hali hii isipotibiwa. Matatizo hayo ni kama yafuatayo:
Mkojo kukosa kutoka kabisa
Wagonjwa wenye tatizo hili lazima wawekewe katheta ili kumimina mkojo.Madhara kwenye kibofu na figo
Kwa sababu ya kibofu kuwa na mkojo wakati wote, ukuta na misuli yake hupanuka na mwishowe hudhoofika hivi kwamba haiwezi kuzuia mkojo.Kwa sababu ya kibofu kujaa
mkojo hurudi kwenye figo na mwishowe huharibu figo.
[emoji23] [emoji23] [emoji23]Akhaaaaaa aoshe mwenyewe,ntasingizia mikono inauma
Mhhh,uchunguzi
Uchunguzi wa ukubwa wa tezi
Uchunguzi huu hufanywa kwa kuingiza kidole chenye glavu nyuma hadi kwenye tezi dume. Daktari huweza kujua ukubwa na hali yake. Iwapo mtu ana ugonjwa huu tezi dume ni kubwa kuliko kawaida, laini na gumu yote pamoja. Iwapo tezi lina vifundo basi inaweza kuwa na kansa (saratani)au inaweza kuwa na kalsium.
Sawa dada , unasomekaVipimo vya picha ya ultrasound na kiasi cha mkojo kwenye kibofu
Picha za ultrasound zinaweza kutathmini ukubwa wa tezi dume na kutambua shida zingine kama kudhoofika kwa tezi,kupanuka kwa njia ya mkojo na kibofu au usaha.Picha hizi pia hutumika kutathmini kiwango cha mkojo unaobaki baada ya kukojoa. Ikiwa kiasi cha mkojo ni chini ya mililita hamsini,basi inaonyesha mkojo wa kutosha unatoka , mililita mia moja hadi mbili au zaidi huonyesha kuna kasoro na basi uchunguzi hufanywe.Kumbuka kipimo cha kidole nyuma na sonografia ni vipimo viwili muhimu kwa utambuzi wa kukua kwa tezi dume.
SawaKipimo cha nambari ya dalili
(Prostate Symptoms Score or index)
Nakusoma, tuendeleeUchunguzi wa maabarani
Uchunguzi huu hauwezi kusaidia katika kutambua ugonjwa wa tezi dume,bali hutumika kutambua matatizo yanayohusiana nao.Mkojo hupimwa ili kutambua maambukizo,na damu hupimwa ili kutathimini uwezo wa figo.Kuna kipimo tofauti cha saratani ya tezi dume.
Aseez sawaProstate Specific Antigen (PSA) hiki ni kipimo muhimu sana cha damu cha kuchunguza saratani ya tezi dume.
SawaUchunguzi zaidi-uchunguzi zaidi ili kutathmini kasi ya mtiririko wa mkojo, uvimbe na matatizo mengine ni pamoja na kuchukua kipande cha tezi dume, IVP,CT urogram,cystoscopynk