Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Mufti Allam anakusudia kutoa tamko maalumu na kuwapa ruhusa maalumu Waislamu wote wanaosafiri kwenda Russia ‘Kuahirisha kufunga kwao’ na hivyo kuwapa leseni wachezaji wa Misri kula na kunywa kwa ajili ya maandalizi mazuri ya Kombe la Dunia. Lakini mpaka Mufti atoe kauli kama hiyo kwa Salah binafsi ndipo staa huyo ataweza kucheza katika pambano la fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya bila ya kufunga Mwezi Mtukufu. Mashabiki wa Liverpool wamekuwa wakitania wanataka kusilimu kuwa Waislamu kwa heshima yake.