Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hata hivyo, Salah na staa mwingine wa Liverpool, Emre Can, kwa sasa watalazimika kuchukua uamuzi mgumu kama Liverpool ikifika fainali ambapo wanaweza kulazimika kucheza wakiwa hawana nguvu zaidi kwa ajili ya kufunga ikiwa ni moja kati ya nguzo tano muhimu za Dini ya Kiislamu.
 
Hata hivyo, hakuna sababu ya kuamiani kuwa Salah, ambaye jina lake linamaanisha ‘Kuabudu’ atakwenda tofauti na imani yake. Mwaka 2014 alikiri alikumbana na wakati mgumu kufunga Mwezi Mtukufu huku akiwa katika maandalizi ya msimu mpya na klabu yake ya zamani Chelsea.
 
Ramadhani ilikuwa ngumu kwangu kwa sababu tulikuwa tunafanya mazoezi mara mbili kila siku, hali ya hewa ilikuwa ya joto na nilicheza kila mechi. Sikuweza hata kunywa maji mpaka saa tatu na nusu usiku. Ingawa nimezoea nimemaliza sasa na ninakula na kunywa kama kawaida,” alisema Salah, staa wa zamani wa Basel ya Uswisi.
 
445211993_334837.jpg
 
Salah ni Muislamu. Anafanya mambo yote ambayo Waislamu wanayafanya. Kabla ya mechi anakwenda kutawadha na kusali, mambo kama hayo. Tunachelewa dakika au dakika mbili kabla ya mechi ili awe tayari kwa ajili ya mechi. Ni yeye, Sadio na Emre Can ndio ambao wanafanya hivyo,” aliongeza Klopp.
 
Ni kitu kizuri. Ni kitu ambacho tunakijitaji katika nyakati hizi. Kumuona kijana mdogo, amejaa mapenzi, amejaa urafiki mwingi, katika dunia ya mihangaiko na mambo mengi yanayotokea katika sayari hii. Mo ni balozi halisi wa Misri na dunia yote ya Kiarabu,” aliongeza Klopp.
 
Ni kitu kizuri. Ni kitu ambacho tunakijitaji katika nyakati hizi. Kumuona kijana mdogo, amejaa mapenzi, amejaa urafiki mwingi, katika dunia ya mihangaiko na mambo mengi yanayotokea katika sayari hii. Mo ni balozi halisi wa Misri na dunia yote ya Kiarabu,” aliongeza Klopp.
 
Ukubwa wa jina la Salah utaweka presha kubwa katika maamuzi yake kuhusu Mwezi wa Ramadhani. Wajasiliamari wamekuwa wakitoa picha zake kando ya ishara ya mwezi mtukufu kutokana na mafanikio yake anayoendelea kuyapata katika soka.
 
Kumekuwa na mawazo mengi katika maamuzi ya kumzawadia kipande cha ardhi. Jinsi ya kufanya hivi itategemea na Mohamed Salah pamoja na mfumo wa Saudi. Kama sheria za Saudi zitaruhusu ardhi imelikiwe na Salah, atapewa kipande cha ardhi katika Mji Mtakatifu wa Makka nje ya Haram. Njia nyingine ya kumuenzi itakuwa ni kujenga msikiti ambao utapewa jina lake,” alisema Fahd al-Rowky
 
Mechi ya kwanza ya Misri katika michuano ya Kombe la Dunia inatazamiwa kuchezwa Juni 15, ikiwa ni siku moja baada ya kumalizika kwa Mwezi mtukufu huku Misri ikishiriki kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990.
 
Mufti Allam anakusudia kutoa tamko maalumu na kuwapa ruhusa maalumu Waislamu wote wanaosafiri kwenda Russia ‘Kuahirisha kufunga kwao’ na hivyo kuwapa leseni wachezaji wa Misri kula na kunywa kwa ajili ya maandalizi mazuri ya Kombe la Dunia. Lakini mpaka Mufti atoe kauli kama hiyo kwa Salah binafsi ndipo staa huyo ataweza kucheza katika pambano la fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya bila ya kufunga Mwezi Mtukufu. Mashabiki wa Liverpool wamekuwa wakitania wanataka kusilimu kuwa Waislamu kwa heshima yake.
 
Back
Top Bottom