Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa mujibu wa Mallya, jiji limekuwa likitumia wastani wa kati ya Sh11.5 milioni na Sh13.5 milioni kila mwaka kuzika maiti za aina hiyo.

Gharama hizo zinahusisha ununuzi wa mafuta na matengenezo ya gari la kubebea maiti, posho kwa wahudumu na wachimba makaburi na sanda za kuzikia. “Pesa hizi hazitoshi ila tatizo kubwa lililotusumbua ni bajeti ya gari la kubeba maiti ambalo sasa tumenunua,” anasema.
 
Imani za dini

Ni ukweli usiopingika kuwa wengi wanaofariki na baadaye maiti zao kutotambuliwa, walikuwa na dini zao kabla ya kufariki dunia na pengine walikuwa na ndoto za kuzikwa kwa kadiri ya heshima na tararibu za dini walizoamini.

Hali si hivyo kwa wale wanaokosa ndugu wa kuomba maiti zao ili wakazike. Wao huishia kuzikwa kibudu.
 
Makaburi yao huchimbwa na watu walioandaliwa na jiji na maiti zinapofikishwa makaburini huwekwa ndani ya makaburi na kufukiwa.

Viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu waliozungumza na gazeti hili wameonyesa kuguswa na hali hiyo, huku wengine wakishauri jiji kukaa nao ili washauriane na kuandaa utaratibu utakaowawezesha kufanya dua kwa marehemu hao.
 
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Khamis Mattaka anasema ni imani ya dini ya Kiislamu kuwa binadamu anapaswa kuthaminiwa na kuheshimiwa akiwa hai au amekufa.

Anakiri kuwa kuna changamoto ya kuhusisha dini kwa maiti zisizojulikana, lakini anaamini kuwa mamlaka za miji zina nafasi ya kukaa na viongozi wa dini na kushauriana nini kifanyike katika kushughulika na maiti za namna hiyo.
 
Hoja iwe ni kuzika na sio kufukia. Hivi ni vitu viwili tofauti kwa sababu maiti anastahili heshima kubwa. Watu wa dini wakikaa na viongozi wa manispaa na halmashauri ya jiji watapata jibu,” anasema Sheikh Mattaka.

Anasema ni vizuri wananchi wahimizwe kutembea na utambulisho kila waendako kwa kuwa wanaweza kufikwa na mauti wakati wowote. Kwa hiyo, wakiwa na utambulisho wataweza kupata mazishi ya heshima badala ya kufukiwa tu.
 
Askofu msaidizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Bukoba, Methodius Kilaini anasema suala hilo huwa na utata na changamoto kubwa kwa kanisa kwa sababu hawajui kama marehemu alibatizwa au la.

“Katika dini, la muhimu si mazishi kwenda mbinguni. Mnaweza kumsaidia kiroho mtu akiwa hai, lakini akifa kama hakutubu haendi kwa Mungu. Kila wakati pia sisi tuna utaratibu wa kuwaombea marehemu,” anasema Askofu Kilaini.
 
Anasema ni vigumu kwa kanisa kumuombea mtu kama hajulikani. “Maiti kama haijulikani sisi hatuwezi kufanya ibada maalumu. Kama hatumtambui hatudai kushirikishwa katika mazishi,” anaongeza.

Kujaa makaburi

Uchunguzi wa Mwananchi katika makaburi ya Mwananyamala kwa Kopa unaonyesha kuwa Halmashauri ya Jiji imekuwa ikipata changamoto kubwa ya maeneo ya kuzika miili hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…