Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Anasema ni vigumu kwa kanisa kumuombea mtu kama hajulikani. “Maiti kama haijulikani sisi hatuwezi kufanya ibada maalumu. Kama hatumtambui hatudai kushirikishwa katika mazishi,” anaongeza.

Kujaa makaburi

Uchunguzi wa Mwananchi katika makaburi ya Mwananyamala kwa Kopa unaonyesha kuwa Halmashauri ya Jiji imekuwa ikipata changamoto kubwa ya maeneo ya kuzika miili hiyo.
 
Maeneo yote ya makaburi ya Mwananyamala, Kinondoni na Temeke ambayo yanajulikana kutumika kuzika maiti hizo yalishajaa miaka kadhaa iliyopita.

Kwa kukosa nafasi, wazikaji wa jiji wamekuwa wakitafuta sehemu za pembezoni mwa makaburi yaliyotumika kuzika maiti zao.
 
Kwa kweli haya makaburi yamejaa siku nyingi na hawa watu wa wanachokifanya ni ku-forge (kulazimisha) tu. Huwa wanatafuta eneo lenye nafuu, wanachimba na kuzika,” anasema mmoja wa vijana wanaoshinda katika makaburi hayo kusubiri vibarua vya kuchimba makaburi.
 
Mallya hakubali wala hakatai kuwa makaburi yamejaa, lakini anakiri kuwa kuna changamoto ya maeneo ya kuzikia maiti za namna hiyo.

“Kuna challenge (changamoto) ya makaburi ya kuwazikia hao. Tumeshaliona hilo na sasa tunachotaka kuhakikisha ni kila halmashauri ina eneo la kuongeza kwa ajili ya huduma hiyo.
 
Anasema siku chache zilizopita iliamuliwa katika kikao kuwa kila halmashauri itenge eneo la kuzikia na mwaka ujao wa fedha watakuwa wameainisha maeneo maalumu kwa ajili ya maziko ya miili isiyotambuliwa.

Manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke zimekwishatenga maeneo mapya ya makaburi ambayo yako nje kidogo ya mji.
 
Ofisa mmoja katika manisapaa ya Ilala anasema wahudumu wa makaburi jijjini Dar es Salaam ni changamoto kubwa.

“We uliza ni nani huwa anachimba makaburi na analipwa na nani?”anasema ofisa huyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

Uchunguzi wa Mwananchi umegundua pia kuwa makaburi yaliyozikwa maiti za watu wasio na ndugu hayawekwi alama yoyote ya utambuzi.
 
Utaratibu wa kujulisha umma

Changamoto nyingine iliyo wazi katika kutafuta utambuzi wa maiti zisizo na ndugu ni kutokuwepo kwa mfumo maalumu wa mamlaka za manispaa kutangaza kwa umma mkubwa kuhusu uwepo wa maiti hizo katika mahospitali ili ndugu waende kuzitambua.

Kwa kawaida, Jeshi la Polisi hutumia viongozi wa serikali za mitaa kuwajulisha watu wa eneo hilo habari za kuokotwa maiti ili waende kuzitambua.
 
Taarifa kama hizo pia hutangazwa katika misikiti na makanisa ili watambuzi wajitokeze.

Mara nyingi taarifa hizo huishia tu katika eneo hilo na iwapo aliyeokotwa ametoka mbali hufanya kazi ya utambuzi kuwa ngumu.

Akijibu swali ni njia zipi wanazotumia kuhakikisha umma unafahamishwa kuhusu uwepo wa maiti isiyo na ndugu, Ofisa uhusiano wa Muhimbili Aminieli Eligaesha anasema: “Maiti nyingi zisizo na utambuzi huletwa hapa na polisi. Tunawahimiza waliopotelewa na ndugu kutembelea mortuary zetu kila wanapopoteza mawasiliano na ndugu zao.”
 
Anasema kwa kawaida maiti hutakiwa kukaa mochwari zaidi ya siku 14 kabla ya kufanya uamuzi wa kuruhusu jiji kuzika. Anasema, hata hivyo, kwa miili isiyofikishwa hospitalini hapo na polisi na iko kwenye hali nzuri, muda wa kukaa mochwari huweza kurefushwa kwa siku 21 hadi 30 kwa matumaini ndugu watajitokeza kutambua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…