Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Raila Odinga amesema maafikiano yake na Uhuru Kenyatta yalioidhinishwa kwa kusalimiana kwa mikono viongozi hao wawili mnamo Machi 9, yamechangia amani na kuruhusu Wakenya kuendelea.
Tangazo la leo litaonekana kama mfano mwingine wa kupatana na kurudi kwa uhusiano mwema baina ya viongozi wawili.
 
Utafiti mpya unaonyesha kwamba robo tatu ya aina zote za viumbe hai waishio kwenye maji yasiyo ya chumvi katika Ziwa Victoria lililopo Afrika Mashariki wamo hatarini ya kuangamia kutokana na uchafuzi wa mazingira na uvuvi uliopindukia.
Hiyo inatishia maisha ya takriban watu milioni 42 wanaoishi Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wahifadhi wa Mazingira wanatoa wito kwa matumizi bora ya ardhi na maji ya ziwa hilo kubwa zaidi za Afrika.
Utafiti huo wa Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Uasilia (IUCN) unaonesha asilimia 20 ya aina zote za viumbehai waliozingatiwa kwenye utafiti huo walibainishwa kuwa kwenye hatari ya kuangamia.
 
Aina nyingi za viumbehai wanaoishi kwenye Bonde la Ziwa Victoria wako kwenye hatari kubwa, hasa kutokana na uchafuzi wa mazingira, matumizi ya rasilimali za kibiolojia (uvuvi uliopita kiasi), kilimo na viumbehai vamizi," ripoti ya shirika hilo inasema.
 
Hatari hizi zimepelekea kiasi cha asilimia 19.7 ya aina za viumbehai wanaoishi kwenye maji baridi kwenye ukanda huu kutathiminiwa kama viumbehai walioko hatarini, na kiasi kikubwa cha kutisha, yaani asilimia 76 ya viumbehai wanaoishi kwenye maji yasiyo ya chumvi wanaopatikana katika ukanda huo pekee, kutathminiwa kama viumbehai walioko hatarini zaidi."
 
Samaki ndio walio kwenye hatari kubwa zaidi ambapo hatari inayowakabili ni kiasi cha asilimia 55.1 ya aina ya viumbehai wote waliotathminiwa.
Wanafuatiwa na kundi la konokono (yaani asilimia 25.5), dekapoda (asilimia 8.3), mimea (asilimia 9.0) na viumbe hai vinavyojulikana kisayansi kama odonata (asilimia 1.9).
Shirika hilo linasema kuna upungufu wa ufahamu wa kutosha kuhusu aina za viumbehai wanaoishi kwenye maji baridi kwa ajili ya kuwezesha maamuzi muafaka kuhusu mazingira na maendeleo kwenye bonde la ziwa.
 
Samaki wa maji yasiyo ya chumvi ni muhimu sana kwa chakula (kwa binadamu na wanyama), na shughuli za uvuvi katika ziwa Victoria usaidia maisha ya kaya za mamilioni ya watu wanaoishi kando kando ya bonde hilo," ripoti ya shirika hilo inasema.
„Mimea inayopatikana ziwani ina matumizi mengi, ikiwa ni pamoja na dawa, chakula, ujenzi na kutengeneza bidhaa za mikono ambazo ni rasilimali muhimu kwa jamii hizi hasa kwa vile jamii nyingi hazipati wala hazimudu bidhaa ghali za sokoni."
 
Back
Top Bottom