Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

4. JE KUNA MIEZI MINGINE AMBAYO HATUIONI?
Sayari ya Dunia ina mwezi mmoja tu. Mwezi wa Dunia una jina lake ambalo ni LUNA. Watu wengi wamezoea kuiita mwezi wa dunia kama "MOON" kwa sababu hapo mwanzoni haikufahamika kama kuna miezi mingine mingi (other moons) zaidi ya huu wa dunia mpaka pale mwanasayansi wa Elimu ya anga GALILEO GALILEI alipogundua miezi mingine mnne (4) ya sayari ya Jupiter hii ilikua mwaka 1610.
Ndiyo kuna sayari nyingi tu kwenye SOLAR SYSTEM yetu zenye miezi zaidi ya mmoja. Miezi mingi ambayo hatuioni, nikisema SOLAR SYSTEM namaanisha JUA pamoja na sayari zake 9 zinazolizunguka.
 
Enhe...lete elimu
 
Karibu kila sayari imezungukwa na miezi yake. Tunaweza kuuona mwezi wa dunia kwa sababu ndio mwezi wake, Dunia ina mwezi mmoja tu ambao tumesema unaitwa LUNA.
Sayari nyingine pia zina miezi yake, mfano sayari ya SATURN imezungukwa na miezi yake 53 baadhi ya majina ya miezi hiyo ya saturn ni MIMAS, PANDORA, TITAN, DIONE, TETHYS, ENCELADUS, RHEA, HYPERION, EPIMETHEUS, PROMETHEUS, PAN, na mengine mengi.
 
Wakati sayari ya JUPITER nayo ina miezi yake 53 inayoizunguka, na Jupiter ndio sayari yenye mwezi mkubwa zaidi kupita miezi yote inayopatikana katika sayari nyingine. Mwezi huo mkubwa wa Jupiter unafahamika kwa jina la GANYMEDE, wanasayansi wanasema mwezi huu ni mkubwa kiasi kwamba unaweza tu kuuona kwa kutumia darubini ya kawaida. Miezi mingine ya Jupiter ni EUROPA, IO (tamka Ayi -oh) na CALLISTO.
Idadi ya miezi inayopatikana katika sayari nyingine ni kama ifuatavyo; Sayari ya URANUS ina miezi 27, Sayari ya NEPTUNE ina miezi 13 wakati sayari ya MARS yenyewe ina miezi 2 tu. Ambayo ni Phobos and Deimos.
Sayari za MERCURY na VENUS hazina kabisa miezi yake.
 
5. JE MWEZI HUWA UNAWAKA NDIO MAANA TUNAUONA MWANGA USIKU?
Mwezi hauna muanga wake. Mwezi ni miamba na vumbi tu. Udongo wa Mwezi upo katika namna ambayo unauwezesha KUAKISI mwanga mwingi zaidi (the moon reflects the sunlight that hits, it reflects more light back towards the Sun than in other directions) unaomulika kutoka kwenye JUA na kuurudisha katika uelekeo wa jua zaidi kuliko uelekeo mwingine.
Mwezi huchukua siku 29 kuizunguuka dunia yetu. Jua linapowaka kwenye uso wa mwezi sisi ndio tonaona mwanga wake kama mbalamwezi.
Mwezi kuonekana umewaka sana au upo nusu inategemeana upo upande gani katika muhimili wake. Ndio mwezi pia unazunguka katika muhimili wake(orbit) huku ukiizunguka dunia
 
[emoji106][emoji106][emoji106]
 
Wakati huu mwezi unaizunguuka dunia kuna wakati sehemu yote inayomulikwa na jua tunaiona hapa usiku - hii ndio kitaalamu huitwa FULL MOOM au mwezi mzima.
Lakini kadri mwezi unavyoizunguuka dunia kuna wakati si sehemu yote ya mwezi inayomulikwa na jua inaonekana upande wetu wa dunia, kuna wakati tunauona Mwezi kama kipande cha kucha iliyokatwa baada ya kuwa upandw wa mwezi unaomulikwa hatuuoni, hapa tunaita MWEZI MCHANGA (NEW MOON) na ndivyo unavyobadilika kutoka mwezi mchanga, nusu na mzima.
 
6. JE MWEZI UPO UMBALI GANI KUTOKA DUNIANI?
Mwezi ndio sehemu pekee nje ya sayari ya Dunia katika ulimwengu ambayo binadamu alisafiri na kuweza kufika.
Tunauona mwezi kwa macho kwa sababu umbo lake ni kubwa, lakini ukweli ni kwamba mwezi upo mbali sana na dunia yetu tofauti na tunavyofikiri. Umbali wa kutoka sayari ya dunia mpaka mwezini ni kilometa Laki Tatu Themanini na Nne Elfu na Mia Nne (384,400 kilometers).
Wanasayansi wanasema umbali huo una eneo linalotosha kuzipanga sayari 30 zenye ukubwa kama wa Dunia na zikaenea katika eneo hilo lililo katikati ya Dunia na Mwezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…