Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

6. JE MWEZI UPO UMBALI GANI KUTOKA DUNIANI?
Mwezi ndio sehemu pekee nje ya sayari ya Dunia katika ulimwengu ambayo binadamu alisafiri na kuweza kufika.
Tunauona mwezi kwa macho kwa sababu umbo lake ni kubwa, lakini ukweli ni kwamba mwezi upo mbali sana na dunia yetu tofauti na tunavyofikiri. Umbali wa kutoka sayari ya dunia mpaka mwezini ni kilometa Laki Tatu Themanini na Nne Elfu na Mia Nne (384,400 kilometers).
Wanasayansi wanasema umbali huo una eneo linalotosha kuzipanga sayari 30 zenye ukubwa kama wa Dunia na zikaenea katika eneo hilo lililo katikati ya Dunia na Mwezi.
 
7. JE KUNA UHUSIANO GANI WA MWEZI NA DUNIA
Wanasayansi wamekubaliana katika hoja kua mwezi ndio unaruhusu maisha ya viumbe hai yaendelee katika Sayari ya Dunia. Hoja hii imeegemea katika mambo yafutayo ambayo Mwezi unaifanyia dunia
(a) Mwezi huvivuta vitu vingi sana vikubwa angani ambavyo huwa vinaelekea kuigonga dunia na ambavyo kama mwezi usingevivuta na vikaangukia katika uso wa dunia basi vingeleta madhara makubwa sana hapa duniani ikiwa ni pamoja na kuua viumbe wote.
Uthibitisho wake ni mabonde makubwa na mashimo yanayopatikana mwezini amabyo yanadhibitisha kwamba yalitokea baada vya vitu vyenye uzito mkubwa kuvuta na kuangukia hapo.(Our moon is basically great attractor of all things that want to hit the Earth).
 
(b) Kupwa na Kujaa kwa Bahari (Ocean Tides) or ( Lunar Tides)
Kupwa na kujaa kwa maji hutokea baharini na pia kwenye maziwa makubwa, mwezi na dunia siku zote huvutana, mwezi huwa unajaribu kuvuta chochote kilichopo duniani ili ikisogeze karibu wakati huo huo dunia nayo huvivuta vitu vyake viendelee kubaki katika dunia. (The Earth’s gravity against The moon's Gravity)
Maji ni kitu kisichotulia sehemu moja na hubadirika umbo kirahisi sana, hivyo mvutano huu huyafanya maji kuelekea kule mwezi ulipo na hapa ndio kitendo cha kupwa na kujaa kwa maji pamoja na mawimbi kutokea baharini.
Kwa wenyeji wa pwani nadhani hali hii ni ya kawaida kwao, kwani kuna wakati fulani ukienda baharini unakuta maji hayapo kipindi cha mchana na mida ya jioni maji hayo hurejea tena
 
(c) Wengine wamejaribu kuhusianisha mwezi na maisha ya watu au viumbe hapa duniani, Dhana hapa ni kuwa kama mwezi unaweza kuvuta maji ya bahari na kuleta kupwa na kujaa kwa bahari( High and Low Tides), basi kwa nini hauwezi kumuathiri mtu ambae asilimia 80 ya mwili wake ni maji?
 
Wengi wanaamini kuwa wakati wa FULL MOON basi wangonjwa kwenye wodi za vichaa (psychiatric wards) wanacharuka sana. Na wakati mwingine tunawasikia watu wakisema fualani kichaa chake kinarudi kila mwezi ukiandama.
 
Wengi wanaamini kuwa wakati wa FULL MOON basi wangonjwa kwenye wodi za vichaa (psychiatric wards) wanacharuka sana. Na wakati mwingine tunawasikia watu wakisema fualani kichaa chake kinarudi kila mwezi ukiandama.
 
Duh!
IMG-20180503-WA0020.jpg
 
Back
Top Bottom