Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pamoja na kutoa maoni yenye utata kuhusu utumwa, kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas imesema haitaachana na rapa maarufu wa Marekani, Kanye West.

“Hatutasema lolote au kubashiri cha kufanya kila wakati wabunifu wetu wa nje wanapotoa maoni yao,” alisema mkurugenzi mkuu wa Adidas, Kasper Rorsted alipoongea na Bloomberg jana Alhamisi.
 
Kanye amekuwa, na ni ni sehemu muhimu ya mikakati yetu, na amekuwa na ubunifu wa aina yake. Na hapo ndipo nitaishia.”

Awali zilianzishwa kampeni za kutaka Adidas iachane na rapa huyo ambaye ni mume wa mtangazaji maarufu wa vipindi vya mazungumzo, Kim Kardashian baada ya kutoa maoni hayo kuwa utumwa ulikuwa ni hiari.
 
Jumanne, West alikuwa na mahojiano katika kipindi cha redio cha TMZ Live na alisema, “wakati unaposikia kuhusu utumwa wa miaka 400 — miaka 400? Hiyo inaonekana ni kama kujitakia.”

Alipobanwa kuhusu kauli hiyo, Rorsted alikiri kuwa "kuna maoni ambayo hatuwezi kuyaunga mkono".

Baadaye akaongeza kusema aliyaona maneno hayo lakini hakuwa amepata muda wa kuzungumza na West.
 
Mkurugenzi huyo hakusema ni kiasi gani West anapata kutokana na ubunifu wake. Katika akaunti yake ya Twitter hivi karibuni, West alielezea jinsi raba yake aliyobuni ya Yeezy ilivyokuwa na faida.

Katika hatua nyingine, mwanamuziki wa rap, Snoop Dogg amesema West wa sasa ni mzungu na kwamba yule wa zamani ameshakufa na kutuma picha aliyoihariri inayomuonyesha rapa huyo akiwa na nywele za kahawia.
 
Mkurugenzi huyo hakusema ni kiasi gani West anapata kutokana na ubunifu wake. Katika akaunti yake ya Twitter hivi karibuni, West alielezea jinsi raba yake aliyobuni ya Yeezy ilivyokuwa na faida.

Katika hatua nyingine, mwanamuziki wa rap, Snoop Dogg amesema West wa sasa ni mzungu na kwamba yule wa zamani ameshakufa na kutuma picha aliyoihariri inayomuonyesha rapa huyo akiwa na nywele za kahawia.
 
Muigizaji na mchekeshaji wa siku nyingi, Amri Athuman maarufu Mzee Majuto leo Mei 4, 2018 amesafirishwa kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua kwa takribani miezi mitatu .



Majuto ameenda India kutibiwa katika hospitali ya Apollo, katika jiji la New Delhi baada ya kusumbuliwa na nyonga iliyosababisha ashindwe kutembea na kupata maumivu makali.
 
Akizungumza na MCL Digital leo, mtoto wake Hamza Amri amesema anaishukuru Serikali kwa kufanikisha safari hiyo, sambamba na wadau mbalimbali waliojitokeza kumsaidia mahitaji mengine.



"Tunamshukuru Mungu pamoja na Serikali kwa kuweza kufanikisha huduma zote za kusafirishwa na za matibabu huko India,” amesema.
 
 
Serikali ya Burundi Ijumaa imetangaza kusimamisha matangazo ya mashirika mawili ya habari ya kimataifa kwa muda wa miezi sita kuanzia Jumatatu ya Mei 7.

Mashirika yanaotarajiwa kuathiriwa na hatua hiyo ni shirika la utangazaji la Sauti ya Amerika (VOA) na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC). Sababu za kusimamishwa ni “kushindwa kuzingatia sheria za utangazaji” na “kukiuka maadili ya kazi”.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…