Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Shinikizo la juu la damu

Shinikizo la juu la damu ambalo kitaalamu huitwa preeclampsia hutokea ghafla kwenye wiki ya 20 ya ujauzito.

Hali hii ikidumu kwa siku chache inaweza kusababisha kufeli kwa figo, kutetemeka mara kwa mara hata kama si wakati wa baridi, kutengeneza jeraha kwenye inina kusababisha matatizo mengine kwenye mfumo wa upumuaji hivyo kuhatarisha maisha ya mhusika.
 
Mjamzito anashauriwa kupunguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na kufanya mazoezi ya mwili ujauzito unapofikisha miezi mitano na kuendelea kujiepusha na shinikizo la juu la damu linaloweza kujitokeza katika kipindi hiki.
 
Kisukari

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za hivi karibuni zinaonyesha kisukari huwapata karibu asilimia 15 ya wajawazito wote. Hali hii hutokea baada ya kondo la nyuma au plasenta ambayo ni mfuko wa unaopitisha chakula na mahitaji mengine kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kuzalisha homoni nyingi zinazozuia insulini kuratibu kiwango cha sukari mwilini.
 
Kwa kawaida, insulini hurekebisha kiasi cha sukari inayoingia mwilini hivyo isipofanyakazi kama inavyotakiwa sukari huendelea kubaki kwenye damu na kumuathiri mtoto aliye tumboni. Mwanamke anashauriwa kutokula vyakula vilivyosindikwa na vye sukari nyingi, kufanya mazoezi mara kwa mara na kufanya vipimo angalau mara moja kwa mwezi kuanzia miezi mitatu ya ujauzito wake ili kudhibiti matatizo yanayoweza kujitokeza.
 
Magonjwa ya moyo

Mfumo mzima wa moyo wa mwanamke hubadilika wakati wa ujauzito. Ujazo wa damu hubadilika pia, mapigo yake huongezeka na shinikizo la damu hupanda.

Mara nyingi mabadiliko haya huwa hayana madhara na wanawake wenye historia ya matatizo ya moyo wakati wa ujauzito wanaweza kuathirika wao na watoto walio tumboni.
 
Takwimu za WHO zinaonyesha kati ya aislimia moja hadi tatu ya wajawazito hupata matatizo haya kutokana.

Japo kiwango hicho ni kidogo lakini ni kupata ushauri na vipimo vya mara kwa mara ili kuepukana na madhara yanayotokana na mabadiliko haya.
 
Anemia

Hili ni tatizo linalojitokeza wakati wa ujauzito kutokana na upungufu wa seli nyekundu za damu. Madini ya chuma ni kitu muhimu sana ili kuasaidia uzalishaji wa seli nyekundu za damu lakini wanawake wengi hawana uhifadhi wa kutosha wa madini chuma mwilini kutokana na sababu za kimaumbile. Mtoto pia anahitaji kiasi fulani cha madini ya chuma.
 
Japo tatizo linaweza kuonekana ni la kawaida, linaweza kusababisha matatizo mengine kama vile kujifungua kabla ya wakati au kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo na matatizo ya ukuaji wa mtoto baada ya kuzaliwa.

Mama mjamzito anashauriwa kula vyakula vinavyoongeza damu kwa wingi kama vile mboga za majani, matunda na nyama nyekundu na kutumia dawa za kuongeza madini ya chuma kuanzia miezi mitatu ya ujauzito hadi wakati wa kujifungua ili kuepuka anemia.
 
Maumivu ya mgongo

Maumivu ya mgongo na kiuno linawapata karibu wanawake wote kwa nyakati toauti. Wajawazito wengi hupata maumivu ya mgongo na kiuno mara nyingi kuanzia muhula wa tatu wa ujauzito yaani mwezi wa sita.

Kwa baadhi tatizo hili huwaletea shida kiasi cha kushindwa kufanya shughuli nyingine. Hii ni kawaida kutokana na mabadiliko ya mwili na maumbile yanayotokea mwilini siku hadi siku wakati wa ujauzito.

Kwa kipindi hiki mwanamke anashauriwa kupata muda mrefu wa kupumzika na anaweza kutumia dawa za kutuliza maumivu lakini ni lazima matumizi ya dawa hizi yaambatane na ushauri wa daktari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…