Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pica

Ni ukweli usiopingika kuwa wajawazito wengi hupendelea kula vitu ambayo kwa mtu wa kawaida hawezi kuvila. Ulaji wa udongo, vitu vyenye asidi na ukakasi mwingi hususan matunda mabichi kama vile maembe malimau na vitu vingine vichachu umekithiri sana kwa wajawazito kutokana na mabadiliko ya mwili yanayosababisha kuvurugika kwa ladha midomoni.
 
Tabia hii inawaweka hatarini wajawazito kupata ugonjwa unaoitwa pica. Huenda ni ugonjwa ambao wengi hawaufahamu ila unaotokana na ulaji wa vitu ambavyo havipo kwenye kundi la chakula ambalo mtu anapaswa kutumia kama mlo.

Wajawazito wapo hatarini zaidi kupata ugonjwa huu kutokana na tabia ya kula vitu ambavyo haviendani na mahitaji ya lishe.
 
Maumivu ya kichwa mara kwa mara

Wajawazito wengi hupata maumivu ya kichwa mara kwa mara hasa katika miezi mitano ya kwanza ya ujauzito yanayoisha mwanzo wa muhula wa tatu, yaani mwanzoni mwa mwezi wa sita wa ujauzito.

Maumivu haya ni kawaida kutokana na mabadiliko yanayojitokeza kwenye mfumo wa homoni na mjamzito anaweza kuyakabili kwa kutumia dawa za kupunguza maumivu baada ya kupata ushauri wa daktari.
 
Wakati mwingine maumivu haya yakidumu kwa zaidi ya miezi sita mfululizo yanaweza kuashiria tatizo jingine kubwa zaidi ya kichwa chenyewe.

Ni muhimu sana kwa wakati huu kupata msaada wa kitabibu ili kubaini tatizo kwa sababu maumivu ya kichwa anayoyapata mjamzito yakidumu kwa muda mrefu yanaweza kuashiria matatizo kama vile uvimbe au kuvuja damu ndani ya ubongo.

Mbali na maumivu ya kichwa, dalili nyingine zinaweza kuwa kutetemeka na mwili kukosa nguvu.
 
Miguu kuvimba

Tatizo hili huwapata karibu wajawazito wote na huwa haliashirii tatizo lolote kubwa la kiafya kwani hutokana na sababu za kimaumbile. Mwanamke huwa na hifadhi kubwa ya maji ambayo baadhi kujitokeza sehemu tofauti za mwili yakiwamo maungio ya miguu.
 
Hali hii mara nyingi hutokea kuanzia miezi mitano ya ujauzito, haimbatani na maumivu yeyote makali wala homa. Ikumbukwe kuvimba hutokea miguuni tu na sio sehemu nyingine za mwili. Lakini hali hii ikijitokeza na sehemu nyingine za mwili hivyo ni vyema kupata kufanya vipimo haraka endapo yatajaa sehemu kwani huashiria figo hazifanyi kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…