Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aliwahi kuniambia huwa anaingiwa na kitu ndani ya nafsi yake kinamsukuma kufanya jambo, lakini baadaye hujutia kufanya kitendo kile,” alisema.

Pili, Mchungaji Patauli anasema Deta alikuwa ameshaanza kuyumba kiroho na alianza kujihusisha na mapenzi, jambo lililothibitishwa na Mama Joshua aliyemnasa na mwanaume ndani ya nyumba yake, Februari mwaka huu.
 
Tatu, baadhi ya majirani ambao hawakupenda kuandikwa majina yao wanasema, Deta alibadilika na alianza kumtesa mtoto huyo kwa muda mrefu wazazi wanapokuwa wametoka.

“Tumeangaliana na dirisha hapa, wakati mwingine unasikia kibao pwaa, halafu mtoto anaanza kulia kwa uchungu, inaweza isishangaze wengi waliomfahamu huyu binti (Deta),” alisema mmoja kati ya wanawake majirani.
 
31108440_1025482207617470_7405816145762058240_n.jpg
Kitu
 
Sura nyingine ya Deta ilionekana kupitia barua yake. Mama Joshua alisema sehemu ya barua hiyo inasomeka: “Mama naomba unisamehe, umenionya sana ila nimekuwa mkaidi, naondoka naelekea nyumbani.”
 
Katika barua hiyo iliyopo katika kituo cha Polisi Kigamboni, Deta amemshukuru mama yake mdogo Magreth kwa kumlea katika shida na raha lakini anajutia kosa la kufanya mauaji hayo.

Baadhi ya majirani walioisoma barua hiyo wanasema barua hiyo ilikuwa na ujumbe mkali wa majonzi ya Deta lakini walishangazwa kwa nini aliamua.
 
Baadhi wanasema pengine ilikuwa ni hofu ya kumuogopa baba Joshua au mapepo yaliyotajwa na mchungaji au ilikuwa ni mwendelezo wa ukatili wa kimya kimya dhidi ya mtoto huyo au ilikuwa hasira za kugombezwa dhidi ya tukio la kujihusisha kimapenzi?
 
Tukio lilivyokuwa

Jumatatu ya kuanzia saa 11 jioni hadi saa saba usiku, Mama Joshua na baadhi ya majirani walianza kumsaka Shafii anayedaiwa kuwa ni rafiki wa kiume wa Deta dakika chache baada ya kukuta barua mezani. Kabla ya kukutana na barua hiyo, Mama Joshua anasema muda wa saa 8:00 mchana alipokea meseji ya Deta, akiwa kazini lakini hakuijibu mapema.
 
Walianza kumtafuta Shafii ili kutoa ushirikiano wa kumpata mtoto baada ya Deta kutuma meseji inayoelekeza kijana huyo kufahamu mahali alipo. Deta alituma namba za simu za Shafii katika simu ya Mama Joshua.

“Nikiwa leba, ananiambia namba ya kaka Shafii ni hii hapa mpigie, sikujua anaitwa jina hilo, nikajiuliza mbona amenitumia namba hizi? Nikashikwa mshtuko, nikaomba ruhusa kazini wakaniruhusu,” alisema.
 
Katika juhudi za kumtafuta baadaye, Deta alipatikana katika simu yake ya mkononi na ndipo alipomjulisha Mama Joshua kwamba arudi nyumbani na mwanaye alimwacha chumbani kwake.

“Nikajiuliza kweli mwanangu tangu Jumatatu yuko ndani tu? Mbona akiwa chumbani anaweza kufungua mlango na kutoka nje?, Nilishtuka, nikamwambia aniletee mwanangu,” alisimulia Mama Joshua kabla ya kumwambia mtoto alimwacha chumbani uvunguni.
 
Mwanasaikolojia, Charles Nduku anasema moja ya sababu ambayo huenda ilichangia binti huyo kufanya mauaji ni mahusiano mabovu na familia.

“Wakati mwingine familia inaweza kumkwaza au kumuumiza mtu kwa kujua au kutojua. Kama ukiumizwa kwa muda mrefu, yale maumivu hujikusanya kwa muda mrefu na kutengeneza sumu ya hasira, kabla ya kufanya tukio kama hilo la mauaji,” anasema Nduku.
 
Back
Top Bottom