Uhai wa Joshua aliyezikwa katika kijiji cha Nyabila, wilayani Sengerema siku ya Ijumaa wiki iliyopita, umekatizwa na mtoto wa dada yake Magreth aitwaye Deta Kalambo (19), aliyekuwa akiishi naye hapo nyumbani kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
“Niliishi naye kwa upendo, sikuwahi kumfanyia kitu kibaya, nilimnunulia nguo nzuri kama mtoto wangu. Nilimjali, nikamsomesha ufundi chereheni, aliingiza mpenzi wake ndani ya nyumba yangu nikamsamehe, sikumuadhibu, leo anamuua mwanangu, ehhee,” anapumua kwa uchungu huku machozi yakimtoka.