Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Kwa mujibu wa Gazeti la Times, gari ya wagonjwa iliitwa nyumbani kwake maeneo ya Cheshire ikiwa ni saa 3:00 asubuhi na kumuwahisha Hospitali ya Macclesfield. Hata hivyo, baadaye alipata rufaa na kupelekwa Hospitali ya Salford Royal. Wachezaji wa Man. United walikwisha taarifiwa hali ya Ferguson kabla ya klabu hiyo kutoa taarifa za kocha huyo kwenye vyombo vya habari na jamii kwa jumla.