Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Meneja wa Brighton Chris Hughton anatarajia uhamisho mwenye utaratibu kuliko wa msimu uliopita wa majira ya joto ambapo wachezaji saba walisajiliwa - sasa klabu hiyo imedhibiti wadfa yake kwenye ligi kuu Uingereza. (Argus)
 
Meneja wa Wales Ryan Giggs anasema anatumai na anaomba meneja wake wa zamani Sir Alex Ferguson ataweza kupona uvujaji wa damu ubongoni.
Ferguson, mwenye umri wa miaka 76, bado yupo katika hali mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura siku ya Jumamosi.
Meneja huyo wa zamani alimruhusu Giggs wakati huo akiwana miaka 17 kucheza kwa mara ya kwanza katika timu ya Manchester United mnamo 1991 na alikuwa katika kikosi cha kwanza cha mechi 13 za Ferguson na kushinda mataji ya Premier League.
 
Daah mie hamna inauma sana bora kujiondokea kimya kimya
Kujiondokea kimya kimya unaweza leta issues nyingi zisizo za lazima. Tungekiona kifo kama sehemu muhimu ya uwepo wetu tungekichukulia kama jambo la kawaida tu na la lazima; na tungejiandaa vizuri kama tunavyojiandaa kwenye ndoa na matukio mengine muhimu maishani.
 
Meneja wa sasa wa Manchester United na mlinzi wa timu ya taifa ya England Phil Jones, pia ametuma ujumbe kama wa Giggs kwamba anamuombea Ferguson na amemtaja kama babake.
Jones alisajiliwa kutoka Blackburn na Ferguson akiwa na umri wa miaka 19 mnamo Juni 2011 na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda cha mechi yake ya mwisho kabla astaafu mnamo Mei 2013 baada ya kushinda mataji 38 katika muda aliyohudumu wa miaka 28 katika klabu hiyo.
"Alinishukulia kama mtoto wake, na lilikuwa jambo la kushangaza," amesema Jones, mwenye umri wa miaka 26.
"Inahuzunisha lakini namjua, na atapambana vilivyo."
 
Tabia za wazungu hizo. Unachagua makaburi na ploti kabisa. Na bima unakata. Na maelekezo yote na nyimbo zitakazoimbwa mpaka na mtu wa kusoma eulogy yako. Inapendeza sana...Unaweza hata kuchimba mkwara watu wasilie...
Hapo kwenye mkwara watu wasilie kwa kabila langu mmmhh! Itakuwa shida, huwa tunajiachia sana kwenye kulia msibani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…