Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kamanda !!!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huku mtaani bei ya mafuta ya kupikia ina paa,baadhi ya maeneo tunaambiwa mafuta hakuna,bungeni waziri wa viwanda anasema nchi ina mafuta ya kutosha tani elfu 90.

Huko bandarini tunaambiwa kuna meli mbili za mafuta zimeshikiliwa na mamlaka ya mapato Tanzania kwa muda wa miezi mitatu sasa..

Tushike lipi,waziri Mwijage anatuambia tuna akiba ya kutosha ya mafuta ya kupikia lakini huku mtaani bei inapaa kila siku.Je kuna hujuma kutoka kwa wafanyabiashara?
 
*HABARI NJEMA KWA WANA UBUNGO DSM*

*UBUNGO MIONGONI MWA HALMASHAURI BORA 17 TANZANIA*

Hayo yamesemwa Leo na *Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Selikali za Mitaa,Mh.Suleiman Jaffo* akitoa Neno la Shukrani Baada ya Meya na Mkurugenzi Ubungo pamoja na Halmashauri zingine kusaini Makubaliano ya Kupokea Fedha kutoka Wizara ya Fedha Mjini Dodoma.

Ambapo *Halmashauri Ya Manispaa ya Ubungo Leo Imepokea Kiasi cha Tsh Billioni 1 kutoka Wizara ya fedha*.Na Kuwa Miongoni Mwa *Halmashauri 17* zilizofanya Vizuri na Kufanikiwa kupitishiwa fedha hizo kwa kukidhi Vigezo baada ya Ushindani wa kuandaa *ANDIKO LA MRADI* kwa kuzingatia fursa za Halmashauri,ambapo Halamshauri zote 185 zilishindanishwa.

*Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Imeandika Mradi Ufufuaji wa Mradi mkakati wa Soko Kubwa la Kisasa katika Soko la Mburahati,Ambapo Ujenzi huo wa Mradi ukipatiwa fedha utasababisha Manispaa ya Ubungo kujitegemea kujiendesha bila kutegemea ruzukuvya serikali kuu ifikapo 2025.pamoja na kuwa Chanzo kikuu cha Mapato na Ajira kwa Watu wa Manispaa ya Ubungo.*

Pichani ni Meya Boniface Jacob na Mkurugenzi wakisaini Mkataba wa makubaliano na Katibu Mkuu wizara ya fedha *Ndugu Dotto James* juu ya kupokea fedha na kuanza Mradi huo kati ya Manispaa na Wizara ya fedha.

*IMETOLEWA* Na
*OFISI YA MSTAHIKI MEYA*
*Manispaa ya Ubungo*
05-May-2018
 
The buck stops here. Kuna mmoja hapo anaujua ukweli...Sema tu wanasiasa hawawezi kusema ukweli sijui kwa nini.
 
Msingi wa maendeleo ni jamii kuwa na hoja kinzani na mwisho wake tunafikia muafaka.Hoja yangu ni hii.

Suala la sheria siku zote halina "option" kama ina ukakasi ni kuifuta na si kutoitekeleza.

1.Suala la nyongeza ya mshahara ni suala la kisheria halina option hili,hoja ya kutoongeza mshahara kwa madai ya ujenzi wa miundo mbinu haiwezi kuwa hoja inayokubalika kwani nyongeza ya mshahara kila mwaka ipo kisheria,kama ilivyo kwa upandaji wa madaraja,vinginevyo bunge liifute ama liibadili sheria hii.

2.Suala la kuijenga,kuilea,kuikuza na kuishirikisha sekta binafsi ni suala la kisera na kisheria,ni wajibu wa serikali kisera na kisheria kuhakikisha sekta binafsi inakuwa sehemu ya injini ya uchumi,ni wajibu wa serikali kisera(2009) na kisheria(2010), kuhakikisha sekta binafsi inakua na kufanya vizuri,vinginevyo bunge liifute kama siyo kuibadili sera na sheria yake.

3.Suala la kuamua pesa hii iende wapi ni moja ya kazi kuu za bunge na siyo mhimili mwingine,sasa mhimili mmoja unapopitisha kisheria pesa hii iende huku halafu mhimili mwingine unajitokeza hadharani na kusema hapana zije huku ni kinyume na sheria.

Tujenge utamaduni wa kuitekeleza na kuziheshimu sheria zetu!.

Mfano suala la uchaguzi ni suala la kisheria,hawezi tokea mtu yeyote akasema nafuta uchaguzi kwani ni gharama sana,mimi
nataka nijikite kwenye maendeleo ya nchi.Hii
ni sheria na sheria haina "option".

Ndiyo maana tunasema mambo ambayo yapo kisheria yasiachwe tu vinginevyo tuzifute sheria zake ama zibadilike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…