Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

"Wewe kama ni mwanafunzi, shule ya msingi umesoma private school, secondary private school, leo uje uchukue fomu ujaze mkopo wakupe mkopo wamekuwa vichaa!!? :- Rais Magufuli

Toa maoni yako
Ukirejea sifa za mwanafunzi kupewa mkopo wa elimu ya juu, nahisi wameainisha kabisa nani apewe kipaumbele katika kupatiwa mkopo huo.

Yatima, wenye ulemavu na wanao toka katika mazingira magumu kiuchumi ndio waotakiwa kupewa kipaumbele katika hilo..Lakini vilevile waweza kuta mwanafunzi kasoma 1° & 2° schools zote private na muda huo huo ni yatima ama ni mlemavu..... Kwa case kama hii nahisi ndo wale wanaopewa asilimia kidogo au kukosa kabisa (ukimuondoa mlemavu)

Uhalisia:- Mara nyingi hata hao waliotoka mazingira magumu wanakosa kabisa, kwa zana ya kwamba bajeti iliyotoka ni kidogo ukilinganisha na idadi ya wanafunzi wanaostahili kupata mkopo..

Maoni yangu:-
Wanabodi watoe mikopo kwa kufuata sifa elekezi, kama mwanafunzi kasoma shule ya kulipa mil.2 -7 kwa miaka 13 kwanini asiweze kulipa mil. 2-7 kwa miaka 3-5???

Kama ni mimi ndo nimesoma private A-Z NISIPEWE MKOPO, ili wasio kuwa na uwezo kiuchumi wapewe....Kwasababu lengo la mkopo ni kumuwezesha mwanafunzi anayetoka katika mazingira magumu kiuchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…