Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

SHABIBY: Waziri Bora Uzuie Pesa, Plan Zenu za Ulaji Tu!

SAA 1 ILIYOPITA

Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby, akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, iliyowasilishwa Bungeni na Waziri mwenye dhamana, mhandisi Isaac Kamwelwe na Naibu Waziri wake Jumaa Aweso.

Video: Msikie Hapa Akifunguka
 
*yule msela wetu aliyenaswa na mahindi kichwani nimepata wazo hivi kwa nini asingetoboa kile kiroba mahindi yamwagike abaki na kiroba tupu halafu angekikata taratibu mpaka kiishe, ila jamaa hakufikiria kabisa mpaka kaaibika....katuaibisha wanaume*



*kila mwanaume alipo amtukane yule jamaa kwa kilugha cha kwenu*[emoji5][emoji5][emoji5][emoji5][emoji5][emoji5][emoji5][emoji5]
Yasingetoka [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Harmonize ataja majina ya wanaume waliotembea na Wolper, Shamsa amvaa

MUUNGWANA BLOG / 2 hours ago




MSANII wa Bongo Fleva, Harmonize ‘Konde Boy’ ameibuka na mpya huku vita baridi kati yake na ex girlfriend wake ambaye ni Staa wa Filamu nchini, Jacqueline Wolper ikizidi kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii.

Kufuatia taarifa zilizopo kwenye mitandao ya kijamii ambapo Wolper ameonekana akitupia madongo heavy Sarah ambaye ni mpenzi wa Harmonize kwa kumuita eti ni ‘Mlezi wa Wana’ kufuatia tsarifa kusambaa kuwa Mzungu huyo kamkacha Harmonize na kuchepukia kwa bodigadi wa Diamond, Mwarabu Fighter.

Sinema la wana likaendelea huku Harmonize akitokwa na povu la OMO kupitia Instagram aambapo alimtetea mpenzi wake Sarah na kusema yeye sio Mlezi wa wana bali Wolper ndo Mlezi wa Wana na kuambatanisha orodha ya wanaume wote aliokuwa nao Kwenye Mahusiano akiwemo mume wa Shamsa Ford, Chid Mapenzi.






Harmonize naye msanii, kagongewa mzungu wake na Romy, kipindi kile kabla hajatoa nyimbo yake ya kwanza alikuwa houseboy kule madale.

Leo hii ananyataaaaaa kweli maisha siyo poa. [emoji23]
 
Mkuu wa BBG Amtaka Nkurunziza Kurejesha Matangazo ya VOA

MASAA 3 YALIYOPITA



Mkurugenzi Mkuu wa Modi ya Marekani ya kuratibu matangazo ya Mashirika ya Serikali, BBG, ambayo inasimamia VOA, John F Lansing.



Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Utangazaji wa Mashirika ya Serikali ya Marekani – BBG – ambayo inasimamia Shirika la Habari la Sauti ya Amerika (VOA), John Lansing, jana Jumatatu alitoa wito kwa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, kubatilisha uamuzi wa serikali yake, wa kupiga marufuku matangazo ya VOA nchini humo, kama njia ya kuimarisha usalama, kuzuia ghasia na kulinda raia wa Burundi.



Kupitia taarifa, Lansing alisema kuwa bodi hiyo itaendelea kuwaunga mkono raia wa Burundi kwa kutoa matangazo ya kuaminika na yasiyopotosha. Taarifa hiyo ilifuatia hatua ya serikali ya Burundi ya kusitisha matangazo ya Sauti ya Amerikakwa muda wa miezi sita nchini humo kuanzia jana Jumatatu.



Hatua hiyo ilijiri siku moja baada ya dunia kuadhimisha siku ya Uhuru wa uandishi wa habari, na siku kumi tu kabla ya kura ya maoni nchini Burundi ambayo huenda ikabadilisha ukomo wa mihula ya urais. Waandishi wa VOA nchini Burundi walithibitisha kwamba sitisho hilo lilianza kutekelezwa kama serikali ilivyokuwa imesema.



“Ingawa VOA pia hutangaza katika mawimbi ya masafa mafupi, televisheni na kupitia mtandao katika nchi hiyo, hapana shaka kwamba matangazo ya redio kupitia masafa ya FM ndiyo maarufu zaidi nchini Burundi,” alisema Lansing.



Aliongeza kuwa raia wa Burundiwamekuwa wakitegemea Sauti ya Amerika kwa matangazo yasiyoegemea upande wowote, wakati nchi hiyo ikikabiliwa na mzozo unaoendelea wa kisiasa na wa kibinadamu.

“Ni muhimu sana kuendelea na matangazo hayo sasa, kuliko wakati mwingine wowote,” alisema afisa huyo mwandamizi.
 
Polisi yawasaka walinzi wa mahakama Iliyowaka Moto Mbeya

Mwakasege Blog / 5 hours ago



Polisi imesema hadi sasa haijajua chanzo cha kuteketea kwa moja jengo la Mahakama ya Mwanzo Uyole jijini hapa na kwamba, inaendelea kuwasaka walinzi wake.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu alisema kwamba jengo la mahakama hiyo na mali zote zilizokuwamo ndani, ziliteketea saa tatu usiku wa kuamkia juzi.


‘Tulipata taarifa kwamba mahakama inaungua tuliwataarifu wenzetu wa zimamoto, lakini wote tulikuta jengo limeshateketea na nyaraka zote zikiwamo pikipiki mbili ambazo zilikuwa ni kielelezo katika moja ya kesi,” alisema Taibu na kuongeza:


“Baada ya kukuta hali hiyo tulijiuliza maswali kadhaa imekuaje. Je, mahakama ile ina walinzi, tukaambiwa inao, bahati mbaya walinzi hawakuwapo wakati huo na hatujui walikwenda wapi?”


Alisema hawajajua chanzo cha tukio hilo hivyo jitihada zinaendelea ikiwamo kuwasaka walinzi hao.


Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Moses Mwidete alisema hakuna kilichookolewa kwa kuwa inaonyesha wakati moto huo unazuka hapakuwapo na mtu yeyote, hivyo nyaraka zote muhimu ziliungua.


“Ulinzi upo na ni walinzi wetu (mahakama), lakini hatujui kilichotokea kwa kuwa mlinzi aliyekuwa zamu hatujui alipo hadi muda huu (jana mchana), kila tukipiga simu yake inaita tu haipokelewi na muda mwingine anakata kabisa simu,” alisema Mwidete na kuongeza:


“Tumeomba wenzetu wa polisi na watu wa mitandao watusaidie kupitia utaalamu wao wa kimtandao kumpata.”


Alisema kazi ya kupata ukweli wa chanzo hicho unaendelea na kitengo cha ulinzi na usalama kupitia ofisi ya kamanda wa polisi mkoa na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji.


“Tumewaomba wenzetu wa zimamoto na polisi kutusaidia hili haraka iwezekanavyo.”

Visit website
 
Jamaa Aliyeiba Mahindi Yakang'ang'ania Kichwani Afikishwa Mahakamani

Mwakasege Blog / 5 hours ago



Mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam, Frank Joseph amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Mlandizi mkoani Pwani akishtakiwa kwa wizi wa mahindi.


Joseph ambaye tukio la kukamatwa kwake liliibua hisia na mijadala mitandaoni ikidaiwa alishindwa kutua mzigo aliodaiwa kuuiba, alisomewa shtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Nabwike Mbaba.


Mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 124/2018 akidaiwa kuiba mahindi debe moja yenye thamani ya Sh20,000. Baada ya kusomewa shtaka, mshtakiwa huyo alikiri kutenda kosa.


Hakimu Nabwike aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 10 ili kupata maelezo ya mlalamikaji ambaye hakuwepo mahakamani.


Licha ya mahakama kumweleza mshtakiwa kuwa dhamana iko wazi na kumpa sharti la kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh500,000, alishindwa kutimiza sharti hilo hivyo alipelekwa rumande.


Tangu Mei 3, Joseph alikuwa akishikiliwa na polisi mkoani Pwani akituhumiwa kuiba mahindi kwa mkazi wa Mlandizi.


Tukio la wizi huo lilivuta hisia kwa jamii baada ya mshtakiwa huyo kudaiwa kushindwa kutua mzigo uliokuwa begani hadi alipokimbilia polisi na mwenye mali kupigiwa simu, ambapo alifika na ‘kumsaidia’ kuutua.

Visit website
 
Back
Top Bottom