Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ali Kiba Aburuzwa Mahakamani

Mwakasege Blog / 1 day ago



Mfanyabiashara wa mitumba Hadija Hassan amefungua kesi ya madai ya matunzo ya mtoto dhidi ya msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba maarufu kama King Kiba.


Katika kesi hiyo, Hadija anadai jumla ya Sh. milioni 1.41, ikiwamo Sh. 950,000 za ada na Sh. 460,000 za matumizi ya mtoto wa miaka mitano (jina limehifadhiwa kwa sababu za kisheria na kimaadili).


Hadija ambaye ni mfanyabiashara wa mitumba amefungua kesi ya madai hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akidai matunzo kwa mlalamikiwa ambaye ni mzazi mwenzie -King Kiba.


Kwa mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa mahakamani hapo, mlalamikaji anadai kuwa Januari, 2013 katika Hospitali ya Mikocheni, jijini Dar es Salaam alizaa mtoto wa kike ambaye baba yake ni mlalamikiwa.


Alidai kupitia hati hiyo kwamba mlalamikiwa anatakiwa kumhudumia mtoto huyo kwa mahitaji yote muhimu ikiwamo chakula, nguo, elimu na matibabu.


"Kutokana na Sheria ya Watoto ya mwaka 2009, mdaiwa anatakiwa kutoa huduma kila mwezi, chakula Sh. 150,000, matunda Sh. 50,000, chakula cha ziada Sh. 50,000, michezo na burudani za watoto Sh. 100,000, nguo Sh. 60,000 na matibabu Sh. 50,000 ambapo jumla ni Sh. 460,000," alidai mlalamikaji kupitia hati hiyo.


Aidha mlalamikiwa anatakiwa kulipa ada ya shule kwa muhula Sh. 950,000, na anadaiwa aliacha kutoa matunzo hayo kwa mtoto tangu Januari, mwaka huu hivyo anaiomba mahakama imwamuru mdaiwa kutoa matunzo hayo ya Sh. 460,000 kila mwezi na ada.


Pamoja na mambo mengine, mlalamikaji anaomba malipo ya kwanza yatolewe mapema baada ya hukumu, na pia anaiomba mahakama imwamuru King Kiba kumsomesha mtoto, kumnunulia nguo na matibabu ikiwamo kumtafutia bima ya afya.


Pia mlalamikaji anaomba mahakama imwamuru Kiba kulipa gharama za matunzo Sh. 460,000 kuanzia Februari 2017 mpaka siku itakapotolewa hukumu na gharama za kesi ziwe kwa mdaiwa.


Mbali na maombi hayo, Hadija anaomba mahakama itoe amri nyingine yoyote itakayoona inafaa kwa manufaa yake. Kesi imefunguliwa kwa msaada wa Kituo cha Wanawake cha Msaada wa Kisheria (WLAC).


Ali Kiba, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Ali Saleh Kiba amefunguliwa madai hayo ikiwa ni siku chache tangu afunge ndoa iliyopendeza mjini Mombasa Kenya.


Visit website
 
Ka Steve Nyerere kametokomea nazo ama?
 
Binti abakwa na kuchomwa moto akiwa hai

Mwakasege Blog / 2 days ago



Polisi wa India wamesema kwamba , msichana wa miaka 16 nchini humo amechomwa moto akiwa hai baada ya wazazi wake kulalamika kwa wazee wa kijiji kuwa binti huyo amebakwa.


Inspekta wa Polisi, Shambhu Thakur alipozungumza na gazeti la Hindustan Times amesema kwamba watu 14 wamekamatwa wakihusishwa na mashambulizi hayo katika Jimbo la Mashariki mwa India Jharkhand.


Kwa mujibu wa Shirika la Habari la BBC, Polisi huyo amesema wazee wa kijiji waliamuru wanaotuhumiwa kuhusika na ubakaji huo walipe faini ya Pauni 550 kama adhabu.


Watu hao walikasirishwa na uamuzi huo na kuamua kuwapiga wazazi wa msichana huyo kisha kumchoma moto binti yao.


''Watuhumiwa wawili waliwapiga wazazi kisha wakakimbilia kwenye nyumba yao wakiwa na washirika wao na kumchoma moto msichana,” Ofisa wa Polisi, Ashok Ram alisema.


Polisi wanasema binti alibakwa na wanaume wawili katika eneo lenye msitu karibu na kijiji cha Raja Kendua baada ya kutekwa akiwa peke yake nyumbani kwao baada ya wazazi wake kuelekea kwenye harusi.


Baada ya tukio hilo wazazi walikwenda kupeleka mashtaka kwa wazee wa kijiji kuwashtaki wabakaji.


Mabaraza ya kijiji hayana nguvu kubwa ya kisheria, hata hivyo yana ushawishi mkubwa kwenye sehemu nyingi ya vijiji vya nchini India katika kusuluhisha migogoro kuliko kutumia gharama nyingi kwenye mfumo wa mahakama.


Polisi katika jimbo hilo wamesema wamewakamata watu 14 kati ya 18 ambao watachunguzwa kutokana na madai ya ubakaji na uuaji.


Visit website
 
...Ukikaidi utapigwa tu (in Mtoto wa Mkulima's voice)
 
Shabiki mmoja mtoto wa Arsenal wakati wote atakuwa anakumbuka mechi ya mwisho ya Arsene Wenger kwenye Uwanja wa nyumbani baada ya Mfaransa huyo kumpa tai yake.

Mtoto huyo mwenye bahati alikuwa jukwaani wakati Arsenal ikishinda mabao 5-0 dhidi ya Burnley Jumapili iliyopita.
 
Alionyesha wazi wanataka kufanya kitu katika mchezo huo wa nyumba mbele ya mashabiki wake.

Mtoto huyo alikuwa jukwaani na bango lake la njano likiwa na maandishi yaliyosemeka: “Tafadhali Arsene, naweza kupata tai yake?”
 
Wenger alionyesha ukomavu wake, kwa kwenda alipo mtoto huyo na kumpa tai nyekundu mbele ya maelfu ya mashabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Emirates kumuaga.

Kocha huyo aliyefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu England mara tatu alifanikiwa kushinda mechi yake ya mwisho nyumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…