Wanawake hao hupeana zamu na wanaume, jana ilikuwa zamu ya wanawake hao ambao bila kujali maji yaliyotuana sokoni hapo pamoja na matope, walionekana wakiendelea na shughuli yao bila wasiwasi wowote.
Mmoja wa wanawake hao, Halima Juma amesema shughuli hizo awali zilikuwa zikifanywa na wanaume pekee kutokana na wanawake kuzuiwa lakini uliibuka mgogoro na kukubaliana kuifanya kwa zamu.
Zaituni Shafikh amesema, “kuna mtu ambaye kazi yake ni kutubebea maji na kutuletea hapa, ndoo moja tunachota kwa Sh500 lakini tunalazimika kumlipa mbebaji Sh200.”
Meneja wa soko hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Obote amesema hiyo ni fursa ambayo watu wameiona na kuichangamkia kutokana na hali ya soko hilo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.