Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni sehemu ya fursa hatuwezi kuwazuia japo mwanzoni walitaka kuleta vurugu tukaamua kuwawekea utaratibu kwamba wafanye kwa zamu, leo wakiosha wanaume kesho wataosha wanawake,” amesema Obote.
 
Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Suleiman Bungara maarufu Bwege amependekeza kuuzwa kwa ndege mbili za Serikali aina ya Bombardier ili fedha zitakazopatikana zitumike kumaliza changamoto za upatikanaji wa maji nchini, kwa madai kuwa zimedumu kwa miaka 57.
 
Bwege ametoa kauli hiyo leo Mei 8, 2018 bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji mwaka 2018/19.
 
Huku akizungumza kwa sauti ya kupanda na kushuka, Bwege amemuomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kusimamia upigaji kura wa wabunge, ili kubaini idadi ya wanaounga mkono ununuzi wa ndege hizo na wale wanaotaka fedha kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya maji.
 
31295471_173330710166502_266296424847638528_n.jpg
 
Leo nakuona kama Spika kweli kweli, upo strong (imara) hongera sana,” amesema na kuwataka wabunge kutoshusha lawama kwa waziri wa wizara hiyo, mhandisi Isaack Kamwelwe na Katibu Mkuu wa wizara, Profesa Kitila Mkumbo kwa madai kuwa bila fedha, hawawezi kufanya lolote.
 
Serikali inatakiwa kutoa fedha za maendeleo maana mnachokisema si mnachokitenda. Leo mwananchi umuulize ndege na maji nini kizuri, nyinyi wabunge kama kweli tuwaulizeni kununua ndege na kuwapa watu maji bora nini?”

Huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge amesema, “wanaosema inunuliwe ndege na wanaosema tuanze maji wasimame, mkirudi mwaka 2020 (baada ya uchaguzi mkuu) mimi sio Bwege. Mheshimiwa Spika uulize, wanaosema ndege na maji halafu tukawaonyeshe huko, mheshimiwa Spika utaruhusu kweli? Wabunge tuwaheshimu mawaziri, sisemi Magufuli mzigo, nasema Serikali ya CCM mzigo.”
 
Back
Top Bottom