Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwigizaji Steve Nyerere amefungukia tuhuma za kutafuna michango ya marehemu Agnes Gerald maarufu Masogange akisema zimehifadhiwa benki kwa ajili ya mtoto.

Akizungumza na MCL Digital leo Mei 9, 2018, Steve Nyerere amesema anayafahamu malalamiko ya ndugu hao kuhusu kutopewa michango lakini ukweli unajulikana na wasanii wote kwa sababu makubaliano yaliwekwa wazi.

“Malalamiko hayo tumeyasikia, kwanza ijulikane kabisa hao wanaolalamika ni ndugu upande wa kiumeni, yaani familia ya mwanaume na sisi ndio tulitangaza kwa umma pale Leders Club kwamba baada ya kukamilisha taratibu zote za safari ya marehemu, fedha hii iliyobaki ni Sh2.1 milioni na tuliwaambia tunamuwekea katika akaunti mtoto wa marehemu,
 
Sasa wanatokea ndugu tu kutaka kukabidhiwa fedha mkononi, nasema hivi hawapewi kama wanavyodai na hakuna michango yoyote iliyoliwa. Kwanza huyo anayelalamika hajui bei ya jeneza wala watu wamemsafirisha vipi marehemu, walichokijua wao ni kulia tu, narudia tena hapewi fedha mtu mkononi hilo wasahau kabisa,” anasema Steve Nyerere.
 
Siku mbili zilizopita, mmoja wa ndugu wa Masogange, aliyejitambulisha kwa jina la Sada alisikika katika kituo kimoja cha televisheni akisema hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa kamati iliyoundwa na wasanii, ambayo pia ilisimamia kwa kiasi kikubwa mazishi ya Masogange.

Sambamba na hilo ndugu hao wamesema kama familia wamejipanga kumlea mtoto huyo kwani walikuwa wanamlea hata wakati wa uhai wa mama yake.
 
Baada ya Agness Masogange kufariki kamati maalumu iliyoundwa na wasanii mbalimbali wa Bongo Movie walichangisha fedha kwa ajili ya kumsaidia mtoto wa marehemu Sania, ili kumsaidia atakapoingia kidato cha kwanza mwakani.
 
Ariana
IMG_20180509_172252.jpg
 
Back
Top Bottom