Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Cardi
IMG_20180509_173235.jpg
 
Okwi afunguka watahakikisha wanashinda mechi zote

MUUNGWANA BLOG / 8 hours ago




MSHAM-BULIAJI wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kusema kuwa watahakikisha wanashinda mechi zote zilizobakia ikiwemo ya Singida United ili kutwaa ubingwa huku akisisitiza hawatajali wanahitaji pointi ngapi.

Simba inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 65, mbele ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 49 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 48.

Simba inahitaji pointi mbili kuweza kutangaza ubingwa huku ikiwa na mechi tatu mkononi kabla ya kumalizika kwa msimu huu.

Akizungumza na Championi Jumatano, Okwi alisema kuwa kwa upande wao wanachokiangalia wakati huu ni kuweza kushinda mechi zote zilizobaki bila ya kuangalia wanataka pointi ngapi.

“Sisi mpaka sasa hivi tunajua tuna mechi tatu, na hatuangalii pointi moja au mbili lakini kikubwa ni kwamba tunataka kushinda mechi zote, tutaendelea kupambana, tunaenda Singida kupamba na kuhakikisha tunapata ushindi ili kuweza kufikia malengo.

“Lakini namshukuru Mungu kwa kucheza mechi nyingi na kuniwezesha kufunga mabao lakini rekodi za watu haziwezi kunipa presha yoyote, nikifanikiwa kufunga katika mechi ijayo itakuwa vizuri zaidi kwa sababu kwetu kikubwa ni timu kushinda,” alisema Okwi ambaye anaongoza kwa kufunga mabao msimu huu akiwa na mabao 20.
 
Kundi la akina mama wa Akashinga wanaleta mabadiliko katika uhifadhi wa wanyama pori Zimbabwe

MUUNGWANA BLOG / 8 hours ago




Zimbabwe ikiwa ni moja ya nchi zinayovutia kutokana na wanyamapori wake inatizamwa kwa jicho baya katika uhifadhi wa wanyama pori hao ikilinganishwa na nchi majirani zake kama Botswana na Afrika Kusini.

Lakini kuna kundi moja la wanawake nchini humo wanaitwa Akashinga kwa maana ya Majasiri au mashujaa ambalo tayari linaleta mabadiliko.
 
Kumetangazwa visa vipya vya ugonjwa wa Ebola vimeibuka DR Congo

MUUNGWANA BLOG / 8 hours ago




Kumetangazwa visa vipya vya ugonjwa wa Ebola kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Kuna visa viwili vilivyothibitishwa na watu 17 waliofariki, wizara ya afya imesema.

Wataalam wa maradhi ya Ebola kutoka wizara ya afya nchini Congo leo Jumatano wanatarajiwa kuambatana na wale wa shirika la afya duniani WHO kwenda jimboni Equateur baada ya kuthibitishwa kuwepo kwa visa hivyo.

Kisa kilichotokea katika mji wa Bikoro kinajiri zaidi ya mwaka baada ya mlipuko wa ugonjwa huo kusababisha vifo vya watu wanne nchini humo, Mnamo 2014 zaidi ya watu 11,000 waliuawa nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia.

Tangazo la kuzuka kwa visa hivyo vipya limetolewa baada ya matokeo ya uchunguzi wa maabara kuthibitisha visa viwili vya Ebola kati ya sampuli za wagonjwa watano waliokuwa wanahsukiwa, Shirika la afya duniani (WHO) limesema.

"Lengo letu kuu ni kuushirikisha mji wa Bikoro na serikali,"Msemaji wa WHO Peter Salam alisema katika taarifa yake.

"Kushirikiana na washirika na kukabiliana na visa mapema katika namna iliyoratibiwaitakuwa ni muhimu katika kuudhibiti ugonjwa huuu hatari."

Shirika hilo la afya duniani linasema limetoa $ milioni 1 kutoka fuko la dharura na limetuma zaidi ya wataalamu 50 kufanya kazi na maafisa nchini Congo, Hii ni mara ya tisa kunazuka ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Virusi vya ugonjwa huo viligunduliwa kwa mara ya kwanza katika nchi hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Zaire, mnamo 1976 na jina lake linatokana na mto Ebola.

Inadhaniwa kwamba Ebola husambazwa katika maeneo ya mbali kupitia popo na husambazwa miongoni mwa binaadamu kutokana na kula nyama za mwituni.
 
Rais Trump atangaza kujitoa katika mkataba wa nyuklia wa Iran

MUUNGWANA BLOG / 8 hours ago




Rais Donald Trump ametangaza kujitoa katika mkataba wa kimataifa wa Nyuklia wa Iran. Ameuita mpango huo kuwa umeoza na ni kero kwa raia wote wa Marekani.

Amesema mpango huo hauwezi kuleta amani hata kama Iran ikikubaliana na kila kitu kama sehemu ya utekelezaji wa mpango huo uliosainiwa mwaka 2015 chini ya utawala wa aliyekuwa rais taifa hilo Barack Obama.

Rais wa Iran amekosoa hatua ya Marekani kujitoa na kudai kuwa haiheshimu makubaliano yake. Akienda kinyume na mataifa ya Ulaya yaliyofikia makubaliano hayo,Trump amesema kuwa watarejhesha vikwazo vya kiuchumi vilivyoondolewa dhidi ya Iran kupitia makubaliano hayo ya mwaka 2015.

Israel na Saudi Arabia kwa pamoja wamepongeza.Viwazo vya vinatarajiwa kuanza dhidi ya Iran ndani miezi mitatu hadi mitatu.

Trump awali alilalamikia mkataba huo kwamba ulikuwa unaiwekea Iran vikwazo kwa muda tu na kwamba ilishindwa kusitisha mpango wake wa makombora na kwamba Iran ilipewa kiasi cha dola bilioni 100 kwaajili ya kutokomeza silaha na ugaidi huko mashariki mwa kati.
 
Back
Top Bottom