Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Miley, Kim, Kylie
IMG_20180509_172651.jpg
 
Mwanasayansi kuuliwa na sindano ya sumu kesho

MUUNGWANA BLOG / 1 hour ago




Mwanasayansi aliyesafiri kutoka Australia mpaka Uswiss David Goodall, kwa ajili ya kuukatisha uhai wake kesho inatarajiwa kuwa ndiyo siku ya kuhitimisha maisha yake ya duniani baada ya madaktari kuchomeka sindano ya sumu katika mshipa.

Kesho, madaktari wanatarajiwa kuweka sindano iliyojazwa dawa ya sodium pentobarbital katika mshipa wa Mwanasayansi huyo mkongwe duniani na kumuacha aisukume mwenyewe kwenda mwilini mwake.

Goodall amelazimika kusafiri kutoka Australia mpaka Basel, Uswisi kukifuata kifo baada ya sheria za kwao kutomruhusu kufanya hivyo.

Akihojiwa na shirika la utangazaji la Marekani CNN, Goodall amesema maisha yake hayana thamani tena ndio maana ameamua kuomba kujiua akiamini hadithi yake itakuwa mfano na kuhamasisha uamuzi kama huo kwa wengine waliochoka kuishi.

Katika mahojiano Goodall amenukuliwa akisema "Natamani ningekuwa na uwezo wa kutembea mashambani na kuona vitu vinavyonizunguka. "Katika umri huu naamka asubuhi, nakunywa chai. Nasubiri mchana nile halafu sina cha kufanya tena. Maisha ya aina hii ya kazi gani?

Goodall aliyezaliwa katika Jiji la London Aprili 1914, anatarajia kufa akiwa na miaka 104 ambapo ameweka wazi kuwa maisha yake yalisimama miaka 10 iliyopita baada ya kupoteza uoni na uwezo wa kutembea na alitamani kama kifo kingemchukua katika miaka hiyo.
 
VIDEO: Tanzania Kushiriki Kombe la Dunia

MUUNGWANA BLOG / 3 hours ago



Shirikisho la mpira Tanzania TFF, leo wamewakabidhi Bendera Timu ya Watoto wanaoishi katika mazingira magumu kutoka mwanza kwenda kushiriki kombe la dunia la mpira wa miguu litakalofanyika huko Moscow, zoezi hili la kukabidhiwa bendera na baraka limefanywa na Rais wa TFF Bw. Wallace Karia katika ofisi za makao makuu ya TFF zilizopo jijini Dar es salaam.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE......................




 
Zitto Kabwe atoa ushauri huu kwa Spika Ndugai

MUUNGWANA BLOG / 5 hours ago




Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Ruyagwa Kabwe amefunguka na kumshauri Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kuwa anapaswa kuwa na msimamo katika kuisimamia serikali kama alivyofanya jana na kudai hii itamfanya aweke 'legacy'

Zitto Kabwe amesema hayo baada ya jana Mei 8, 2018 Spika wa Bunge kumtaka Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage kuja na maelezo ya kutosha kuhusu tatizo la sukari na mafuta nchini baada ya kutoridhishwa na majibu ya waziri huyo bungeni na kusisitiza kuwa haiwezekani wananchi wakawa wanaumia kwa gharama kubwa ya bidhaa hizo.

"Namna ambavyo Spika Ndugai amesimamia suala la majibu ya Serikali kuhusu kadhia ya Sukari na Mafuta ya Uto (kula) inanikumbusha bunge la tisa. Ndugai sasa ameanza kuweka ‘legacy’ yake. Aendelee hivi hivi ila jambo la muhimu zaidi suala la mafuta litazamwe kwa muktadha wa Wakulima wa Mawese na Alizeti" alisisitiza Zitto Kabwe

Kutokana na Spika wa Bunge na bunge kiujumla kutoridhika na majibu ya Waziri Mwijage hivyo spika wa bunge Job Ndugai aliomba maelezo zaidi na kutaka swali hilo kuulizwa tena wiki ijayo ili serikali ije na majibu ya kueleweka na yenye tija.
 
Mama mmoja alala nje baada ya nyumba yake kufungwa

MUUNGWANA BLOG / 5 hours ago




Mama mmoja ajulikanaye kwa jina la Editha Wambura, amejikuta akilala nje jana mara baada ya taasisi inayojishughulisha na udalali hapa nchini, YONO kuifunga nyumba yake yenye namba 58, iliyoko Kata ya Mikocheni mtaa wa Mpungani, huku wakidai agizo hilo limetoka RITA .

Tukio hilo la kutolewa mama huyo nje, lilitokea jana jioni huku chanzo cha kufungwa kwa nyumba hiyo kikidaiwa ni zuio kutoka kwa ndugu wa marehemu ambao wanashirikiana na yo RITA ambao ndio wasimamizi wa Mirathi huku wakiamuru YONO kufungia Nyumba hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo asubuhi kwenye eneo la Nyumba hiyo, Editha Wambura, ambaye ni mke wa Marehemu ,James Wambura, amesema chanzo cha mgogoro huo ilitokea mara baada ya mumewe kufariki na kuacha baadhi ya mali ambazo ndugu zake walijitokeza na kuzidai.

Amesema kuwa, baada ya kufariki mumewe mwaka 2012, kuliibuka mizozo mbali mbali huku ndugu wa mume wakimletea baadhi ya wanawake wakidai amezaa nao watoto 11.

Aidha, amesema kabla ya mumewe kufariki hajawahi kuwaona hao watoto lakini leo analetewa, miongoni mwa wakina mama waliowaleta watoto hao ni pamoja na wafanyakazi wa Bar na mwalimu ambaye alimfundisha mtoto wake alivyokuwa chekechea.

"Nashangaa sana ndugu waandishi, mimi na mume wangu tumefunga ndoa 1995, mpaka sasa tumebahatika kupata watoto 3, mmoja yupo darasa la saba na wengine wapo chuo mwaka wa kwanza, kwani nini leo wanaletwa hawa, kuna namna hapa inafanyika kunidhurumu mali zangu nahangaika sana na hawa watoto nalipia ada, kula na maradhi juu yangu je wakichukua na hii mali iliyobakia tutaishi vipi?"aliuliza mama huyo akionekana na uchungu mkubwa sana.




Ameongeza kuwa, mpaka sasa wana miaka 18 katika nyumba hiyo wanaishi hapo, amekuwa mtu wa kufuatiliwa sana na Yono pamoja na Rita, amesema Rita ndio wasimamizi wa Mirathi lakini hawatendi haki wanaangalia upande wa ndugu wa marehemu, Mahakama haijatoa idhini yoyote ya kuondoka kwenye nyumba hiyo, kwanini wao wamechukua majukumu ya kumtoa nje? hii ni mara ya pili kuchukua vitu vyake vya ndani na kununua upya, hivyo amesema kuwa watu hao wanafanya unyanyasaji kwani hawafuati sheria wamekuwa watu wa kutumia nguvu pasipo na haki kutendeka.

Pia ametaja baadhi ya mali ambazo amechukuliwa, miongoni mwa mali hizo ni pamoja na fedha, magari 2, vifaa vya Ofisi, Msasani klabu, Trekta 2.

Mama huyo amesema kuwa, alitegemea RITA wangekuwa msaada kwake lakini cha kushangaza wao ndo wanamnyanyasa wakati kesi hiyo bado ipo Mahakama Kuu na haijatolewa ufumbuzi.

Ameiomba Serikali ya Rais Magufuli, Wairi husika wa Sheria na Wairi wa Ardhi, M kuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na Mkuu wa Wilaya kuingilia kati na kuhakikisha kwamba anapata haki zake zote ikiwemo zile walizochukua mwanzo.

Hata hivyo, kaimu Meneja wa masuala ya ufilisi na udhamini, RITA, Reinald Makoko, amesema kuwa kuhusiana na suala zima la usimamizi wa mirathi ya Marehemu James Wambura, ni kwamba waliteuliwa na Mahakama kuu tarehe 23/5/2014 kusimamia mirathi hiyo mara baada ya mgogoro baina ya warithi kutokuafikiana,hivyo Mahakama ikaona kwamba kabiziwasi mkuu ndiye mtu pekee ambaye anawea kusimamia mirathi hiyo.

Hivyo baada ya kufuata sheria jana wakafanikiwa kumuondoa mama huyo kwenye hiyo nyumba kuhakikisha inauzwa au kupangishwa ili warithi wote waweze kupata stahili yao.

"Mamama huyo sio mrithi, ni mtalaka wa muda mrefu wa Marehemu, lakini ana haki ya kufuatilia sehemu ya mirathi hiyo ambayo ni stahili ya watoto wake watatu aliozaa na Marehemu, hivyo ilikuwa ni sahihi kumuondoa kwenye nyumba hiyo ili haki itendeke kwa warithi wote ikiwemo watoto alionao yeye"amesema Mkoko

Hivyo ametoa wito na kusema upo umuhimu wa kuandika wosia kwa sababu itasaidia sana kuepusha migogoro ambayo inaweza kutokea baada ya mtu kufariki, hususani ni pale panapokuwa na warithi wengi au warithi mbali mbali wanaotoka kwenye matumbo tofauti, kwa mfano baba amezaa na wanawake wawili wale watoto kukaa pamoja na kuelewana ni vigumu , hivyo tunawakaribisha wananchi kuja kwa ajili ya kuandika wosia kwa sababu Ofisi hiyo inaandika wosia kwa manufaa ambayo warithi watapenda mtu anufaike baada ya marehemu kufariki dunia.
 
Steve Nyerere afunguka kuhusu michango ya msiba wa Agness Masogange

MUUNGWANA BLOG / 5 hours ago




Msanii wa filamu bongo ambaye pia ni mchekeshaji maarufu Steve Nyerere, amefunguka juu ya tuhuma za kutofikisha fedha za michango zilizobaki kwenye msiba wa Agness Masogange, na kusema kuwa pesa hizo haziwezi kupewa familia.

Akizungumza na www.eatv.tv Steve Nyerere amesema kwamba pesa hizo ambazo zimetajwa kuwa milioni mbili zimekusudiwa kumsaidia mtoto wa marehemu Sania, atakapoanza kidato cha kwanza hapo mwakani,

Steve Nyerere ameendelea kwa kusema kwamba familia ya Agness inapaswa kushukuru kwa mchango wao walioutoa kumzika ndugu yao, na sio kuanza kuulizia masuala ya pesa, kwani pesa hizo si kwa ajili yao bali ni kwa ajili ya mtoto.
 
Mechi ya Yanga kuchezwa Usiku

MUUNGWANA BLOG / 5 hours ago




Mabingwa wa soka nchini na wawakilishi pekee wa kimataifa klabu ya Yanga, wanatarajia kucheza mchezo wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya Rayon Spots, mchezo ambao utapigwa saa 1:00 usiku.

Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Yanga na Rayon Sports ya nchini Rwanda utachezwa Mei 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Shirikisho la soka nchini (TFF) mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Angola na tayari shirikisho la soka Africa (CAF), limeshaitumia Yanga na TFF majina ya waamuzi na kamisaa wa mchezo.

Yanga ilicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya U.S.M Alger wikiendi iliyopita nchini Algeria na kukubali kipigo cha mabao 4-0. Matokeo ambayo yameifanya kushika mkia katika kundi D.

Kundi hilo linaongozwa na U.S.M Alger yenye alama 3, ikifutiwa na Gor Mahia ya Kenya yenye alama 1 sawa na Rayon Sports yenye alama 1. Baada ya mechi ya Rayon Sports Yanga itacheza na Gor Mahia.
 
Back
Top Bottom