Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2018-05-07-23-13-35.jpg
 
Usafiri wa anga (ndege) unaaminiwa kuwa miongoni mwa usafiri salama zaidi na kwamba uwezekano wa kupata ajali na kufariki unapotumia usafiri huo ni ndogo sana ikilinganishwa na usafiri mwingine. Licha ya kuwa uwezekano huo ni mdogo, lakini mara kadhaa ajali hutokea na watu hupoteza maisha.
 
Je, unafahamu kuwa vifo hivyo ambavyo vimetokana na ajali za ndege, wakati mwingine vingeweza kuepukika? Lakini kabla hatujafika mbali katika kueleza mambo mbalimbali unayoshauriwa kufanya unapokuwa kwenye ndege iliyopata hitilafu, ni vyema tufahamu kuwa, ajali za ndege hazifanani, hivyo hakuna mbinu moja inayoweza kutumiwa katika ajali zote.
 
Mfano, uwezekano wa watu kupona katika ndege inayoanguka kwa kutanguliza pua chini ni ndogo sana, kwani baada ya kugonga ardhi mara nyingi ndege hizo huwaka moto. Lakini ifahamike kuwa, ajali nyingi za ndege huwa haziwi za namna hii.
 
Kaa mwisho wa ndege

Sehemu unayokaa wakati ndege imepata hutilafu, kwa kiwango kikubwa inaathiri uwezo wako wa kupona. Takwimu kutoka Federal Aviation Administration (FAA) ya nchini Marekani zinaonesha kuwa, wanaokuwa wamekaa mbele au katikati wakati ndege imepata hitilafu, wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kufariki kuliko waliokaa nyuma.
 
Back
Top Bottom