Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sikiliza maelezo ya wahudumu na soma vipeperushi vya usalama

Watu wengine kwa vile wamekuwa wakisafiri kwa ndege mara kwa mara, huona kama wamezoea maelekezo yanayotolewa na wahudumu wa ndege, na hivyo kuamua kutokusikiliza. Lakini ni vyema ukasikiliza maelekezo hayo ambayo hutolewa mara zote kabla ya ndege kuanza safari.
 
Mavazi yanayotakiwa ni kama vile jeans, tisheti, jacket na nguo hizo ziwe za pamba (cotton) ili kuhakikisha kwamba haziyeyuki kirahsi na kukusababishi matatizo mengine.
 
Unapokuwa kwenye ndege, soma vipeperushi vyote vinavyoeleza kuhusu usalama wa abiria, na uweke makakati wako wa namna ya kutoka nje ya ndege tatizo likitokea. Usisubiri hadi pale tatizo litokee, kwani hautakuwa na muda wa kufanya mipango hiyo.
 
Sheria ya dakika +3 na -8

Mara nyingi sana, ajali za ndege hutokea muda mfupi baada ya kupaaa au wakati inatua. Mara nyingi huwa ni dakika tatu baada ya kupaa, au dakika nane kabla ya kutua.
 
Ili kuhakikisha unakuwa salama, unatakiwa kuwa makini muda huu kuhakikisha kwamba hausikilizi mziki, haulali, hauvui viatu au kufanya kitu chochote kitakachokufanya usiwe makini kufuatilia mwenendo wa ndege. Kuwa macho na tayari kutekeleza mpango wako wa kujiokoa endapo tatizo litatokea.
 
Kuwa mkakamavu

Sasa upo kwenye ndege, na tayari wahudumu wameshatangaza hatari kuwa ndege imepata hitilafu, nini unatakiwa kufanya? Wataalamu wa usafiri wa ndege wameeleza kuwa, unatakiwa kutoa vitu vyenye ncha kali mfukoni mwako kama vile funguo, kalamu, penseli na pia unashauri kutoa mizigo iliyopo mbele yako ili isikuzuie wewe au wengine kutembea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…