Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Biashara mpya nyingi huanzishwa kila mwaka wakati, nyingine zikifungwa kutokana na sababu mbalimbali. Lililo wazi kwa wanaoshindwa kuziendesha ni kutokuwa makini kwenye baadhi ya mambo muhimu.
 
Unahitaji huduma za mwanasheria kufanikisha mambo yako mengi hasa mikataba ya kibiashara. Inategemea uwezo na ukubwa wa biashara, lakini unalazimika kuwa na mwanasheria ambaye atakuwa anakusaidia kuandika barua na mikataba ya kibiashara ili kuepuka mgogoro hapo baadaye hata kushinda kesi endapo zitakuwepo.
 
Mshauri wa biashara ni muhimu hasa unapokuwa na shida mbalimbali. Shida hizo ni kama vile upungufu wa wateja, kupata hasara, mafunzo ya wafanyakazi, kuandaa mipango ya biashara na kutathmini mwenendo wa biashara na namna ya kukabiliana na ushindani sokoni.
 
Hata kama biashara yako ni ndogo, unatakiwa kuwa na mhasibu au huduma zake kwa ajili ya kuandaa mambo mengi yakiwamo makadirio ya kodi. Wataalamu hawa unaweza kuwakodisha kwa muda wakusaidie kuweka sawa kumbukumbu za fedha za biashara.
 
Hakikisha fedha za biashara zinahifadhiwa benki kwa usalama. Chagua benki yenye faida, iliyo karibu na isiyo na usumbufu. Zipo benki nyingi kila kona.
 
Bima ni muhimu katika kupunguza uwezekano wa kukabiliana hasara inayoweza kujitokeza. Kuna kampuni nyingi za bima, achagua uipendayo. Bima husaidia kukabiliana na hasara katika biashara.
 
Leseni na vibali vyote vinavyohitajika huthibitisha biashara yako imefuata utaratibu na sheria za nchi. Lipia leseni ya biashara na vibali mbalimbali kwa mujibu wa sekta uliyomo kwani kupuuzia hili kutakuletea usumbufu hata kufungiwa biashara yako. Watumie wataalamu wa biashara katika hilikuepuka usumbufu.
 
Ukiwa mjasiriamali na mfanyabiashara usijitenge na umoja au ushirikisho naa wafanyabiashara. Kujiunga huko kuna faida nyingi ikiwamo kujuana na watu wenye malengo kama yako, kujua fursa za uwekezaji, kupata mafunzo na misaada ama maelekezo ya kisheria na fedha.
 
Back
Top Bottom