Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baada ya muda mfupi tu, maadui wa Galileo walianza kudai kwamba kitabu chake kinamdhihaki papa. Akiwa ameshitakiwa kuwa mzushi wa kidini na kutishiwa kuteswa, Galileo alilazimishwa kukataa mafundisho ya Corpenicus.
 
3aa51dc9-472d-4e49-a566-5c6e50c383c1.jpg
 
Katika mwaka wa 1633, Baraza la Kikatoliki la Kuhukumu Wazushi, lilimhukumu kifungo cha kudumu cha nyumbani, na kupiga marufuku vitabu vyake. Galileo alikufa akiwa nyumbani kwake katika mji wa Arcetri, karibu na Florence, Januari 8, 1642.
 
Papa John Paul wa Pili, alikubali kwamba Kanisa Katoliki lilimhukumu kimakosa Galileo
Kwa mamia ya miaka, baadhi ya utafiti wa Galileo uliendelea kuwa katika orodha ya vitabu ambavyo Wakatoliki hawakuruhusiwa kusoma.
 
Hata hivyo, katika mwaka wa 1979, kanisa hilo lilichunguza tena hatua iliyochukuliwa na Baraza la Kikatoliki la Kuhukumu Wazushi miaka 300 iliyopita. Mwishowe, katika mwaka wa 1992, Papa John Paul wa Pili, alikubali kwamba Kanisa Katoliki lilimhukumu kimakosa Galileo.
 
Back
Top Bottom