Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

tujifunze kitu kuhusu uatamishaji na utotoleshaji wa vifaranga maana hili ndilo limekuwa eneo muhimu kifugaji maana hapa ndipo panapotupatia mbegu kwa ajili ya kuendeleza ufugaji wetu. Matokeo ya kifugaji huanzia na maendeleo na namna ambavyo kifaranga kimeweza kuzalishwa iwapo kifaranga kitazalishwa kwenye mazingira yasiyokizi vigezo ni wazi hata ukuaji wa kifaranga hiki utakuwa ni adimu na wenye kusuasua na matokeo yake kuwa kipingamizi kwa mfugaji. Mazingira bora dhidi ya kifaranga yanahitajika tangu kifaranga kinaanza hatua zake za ukuaji tokea kiini kinaanza kujengwa na kukua ni wazi kwenye hatua hii ya ukuaji iwapo hazitozingatiwa ipasavyo kufuata kanuni za ufugaji bora ni wazi itaathiri hatua nyingine za ukuaji wa kifaranga hadi kuwa kuku kamili.
 
Kifaranga kilicho bora ni matokeo ya kuku wazazi walio bora yaani waliolishwa ipasavyo na kupewa chanjo zote zinazostahili na kwa wakati. Afya ya kuku wazazi,umri wao walionao na namna ya ulishwaji wao ni vigezo vikuu na muhimu kwenye kukupa matokeo ya kifaranga chenye afya bora na kinachoweza kukupa matokeo bora kabisa.
 
VIGEZO VYA UCHAGUZI WA MAYAI YANAYOANDALIWA KWA AJILI YA KUTOTOLESHWA.
Sil kila yai linalotagwa na kuku basi linakidhi sifa na vigezo vya kutotoleshwa ni wazi kuwa kama yai halikidhi vigezo vya kutotoleshwa na kuwa kifaranga hata uwezekano wa kutototoleshwa wenyewe unakuwa haupo.Wafugaji wengi tumekuwa tukikusanya mayai hovyo hovyo na kuyapelekwa kutotoleshwa bila kuzingatia vigezo hivi muhimu;-
 
A) YAWE YAMERUTUBISHWA NA JOGOO.
Sifa kuu na muhimu ya utotoleshwaji wa mayai ni kuwa ni lazima yawe yamerutubishwa na kuku mwanaume kwa uwiano stahili wa majogoo na mitetea na uwiano unaopendekekzwa ni wa mitetea nane kwa jogoo mmoja.
 
B) YAWE NA GANDA SAFI LISILO NA UFA.
Mayai yanayoandaliwa kwa ajili ya kutotoleshwa ni lazima yawe na ganda safi lisilo na uchafu uiogandia.Usafi wa mayai unategemea pia na usafi wa abandani na mahali ambapo kuku wanatagia. Iwapo kuku watakua na miguu misafi na wanataga kwenye viota visafi na ukusanyji wa mayai unafanywa kwa wakati na kuwekwa kwenye chombo kisafi ni wazi hata mayai yatakuwa safi kabisa na salama tofauti na vinginevyo.
 
C) YAWE NA UKUBWA, MAUMBO NA RANGI ZINAZOWIANA.
Mayai yanayoweza kukupa matokeo sahihi ni yale yaliyo na ukubwa unaowiana,maumbo yanayofannana na rangi zinazo fanana usichukue mayai yenye ganda lenye vinundunundu, yasiyo na shape isiyoeleweka,yenye viini viwiwli au mayai yenye nyufa. nauzito unaopendekezwa ni wa 50g-70g. Kutokana na ukweli kuwa mayai madogo yanatotolewa mapema kuliko makubwa ni wazi kuwa mayai madogo yaanze kuatamishwa masaa 8-18 baada ya mayai makubwa kuanza kuatamiwa.
 
D) YASIWE YAMEHIFADHIWA ZAIDI YA SIKU SABA TANGU KUKUSANYWA.
Ili kupata utotoleshwaji wenye tija ni lazima mayai yanayototoreshwa na kuwekwa kwenye mashine yawe yamehifadhiwa kwa kipindi kisichozidi siku saba kabla ya kuanza kuatamiwa.
 
E)YAHIFADHIWE SEHEMU YENYE JOTO STAHILI NA KIASI.
Mayai yanayoandaliwa kwa ajili ya kuatamishwa ni lazima yahifadhiwe kwenye chumba kisichopitisha upepo mkali na chenye nyuzi joto 12.8 sentigredi na 15.6 sentigredi na unyevuunyevu wa asilimia 75 hadi asilimia 80.
 
F) YAKUSANYWE SEHEMU YENYE NCHA KALI IKIANGALIA CHINI.
Kipindi cha ukusanyaji wa mayai mayai yanayokusanywa ni lazima yakusanywe sehemu iliyochongoka ikiangalia chini,mayai yayiyohifadhiwa kwa namna hii hayahitaji kugeuzwa geuzwa.
Uatamishaji wa mayai huweza kufanywa kwa kutumia njia mbili yaani kwa kutumia kuku wazazi kuweza kuyalalia mayai au kwa kutumia mashine inafahamika kama incubator.
 
Back
Top Bottom