Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UATAMISHAJI NA UTOTOLESHAJI WA MAYAI KWA KUTUMIA MASHINE MAALUM (INCUBATOR).
Uatamishaji wa mayai kwa kutumia mashine maalumu hufanywa kwa kifaa maalum ambacho hujulikana kama incubator. Incubator zipo za aina mbalimbali na ukubwa tofauti tofauti kuhlingana na mahitaji ya mtfugaji. Kifaa hiki ni muhimu kwa mfugaji ili kuweza kuzalisha vifaranga vyenye ubora. Incubator ni vyema ikatumiwa kwa kuzingatia masharti maalum ili kuweza kupata matokeo yenye tija iwapo kama kifaa hiki hakitosimamiwa ipasavyo huweza kuwa chanzo kimojawapo cha maradhi sugu kwa kifaranga.
 
MAMBO YA KUZINGATIA KWENYE UATAMISHAJI WA MAYAI KWA KUTUMIA MASHINE:
A)KIASI CHA JOTO.
Mayai yanayototoleshwa kwenye mashine huifadhiwa kwa kiwango maalumu cha joto kinachozalishwa na mashine kiasi cha 25-30 BC. Ukuaji wa kiini tete (embryo) hutegemea kiwango maalum cha joto iwapo kiwango kicho cha joto hakitozingatiwa ni wazi hata kiasi cha mayai yatakayototoleshwa hakitoridhisha kutokana na embryo nyingi kufa.
 
B)KIASI CHA UNYEVU UNYEVU NDANI YA MASHINE.
Kipindi cha uatamiaji wa mayai mayai hupoteza 11-12% ya uzito wake kutokana na kupteza unyevu, kiasi cha unyevu kwenye incubator ndicho kinachosaidi kuweka sawa uwiano wa unyevu kwenye mayai. Upotevu mkubwa wa kiwango cha unyevu kwenye mayai katika hatua za mwazo za ukuaji hupelekea kiini tete kufa na hatimaye yai kuharibika.
 
C) KIASI CHA HEWA KINACHOINGIA NA KUTOKA NDANI YA MASHINE.
Kiasi cha unyevu,oksijeni, na carbondioxide kinachoingia na kutoka ndani ya mashine ni jambo la muhimu kabisa, hii ni kutokana na ukweli kwamba kiini tete kinachokuwa uhitaji oksijeni na kutoa carbondioxide na unyevu hiyo kiasi cha unyevu na carbondioxide kisipo ruhusiwa ipasavyo huweza kusababisha kufa kwa kiini tete.
 
D)NAMNA MAYAI YALIVYOKAA NA KUGEUZWA KWENYE MASHINE.
Ili kupata utotoleshaji wenye tija ni wazi ni lazima mayai yawe yanageuzwa kwenye namna ambay hayatoruhusu kiini tete kushikana na ganda la yai, ugeuzwaji wa mayai kwa kutumia mikono kwenye incubator ndogo ni lazima ufanywe kwa kuhakikisha mikono inakuwa misafi ili kuzuia bacteria kuingia kwenye yai.
 
E)UCHAGUZI NA UHIFADHI SAHIHI WA MAYAI BORA.
Ili kupata matokeo bora ya kifaranga ni lazima mfugaji azingatie upatikanaji wa mayai yaliyo bora yaliyotagwa na kuku mzazi mwenye afya na yaliyorutubishwa na jogoo lenye afya na linalofaakwa mbegu ifahamike pia si kila yai linalotagwa na kuku linafaa kutoa kifaranga chenye ubora.
 
E)UCHAGUZI NA UHIFADHI SAHIHI WA MAYAI BORA.
Ili kupata matokeo bora ya kifaranga ni lazima mfugaji azingatie upatikanaji wa mayai yaliyo bora yaliyotagwa na kuku mzazi mwenye afya na yaliyorutubishwa na jogoo lenye afya na linalofaakwa mbegu ifahamike pia si kila yai linalotagwa na kuku linafaa kutoa kifaranga chenye ubora.
 
F)USAFI.
Mayai kwa ajili ya kutotolesha vifaranga vyenye ubora ni lazima yawe masafi,yamekusanywa na kuhifadhiwa kwenye vyombo visafi na yatakayowekwa kwenye incubator safi iliyo kwenye chumba kisafi. Usafi ni jambo la muhimu sana kwenye kupata kifaranga chenye ubora na kisicho na maambukizi yoyote ya bakteria
 
G) KUNYUNYIZA DAWA ZA FUMIGATION KWA USAHIHI.
Mashine ya kutotolesha mayai inapaswa kusafishwa kwa dawa maalum mara kwa mara ili kuzuia kuzaliana na kukua kwa bakteria kwa kiwango kikubwa.Dawa hizi ni lazima zinyunyizwe kwa usahihi kabisa ili kufanya kazi inavyostahili.
 
Back
Top Bottom