Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya Famasia katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), amekutwa amekufa chumbani.

Taarifa kutoka chuoni hapo zinasema mwili wa mwanafunzi huyo, Edward Kahitwa ulikutwa chumbani jana Mei 19, 2018.

Imeelezwa Kahitwa hakuonekana hadharani tangu Alhamisi Mei 17, 2018 hadi mwili wake ulipogundulika kuwapo chumbani jana.
 
Alipotafutwa na mwandishi wa habari wa The Citizen, Ofisa Uhusiano wa Muhas, Hellen Mtui alithibitisha kifo cha Kahitwa na kueleza kuwa chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana.

Tayari Kaimu mshauri wa wanafunzi Muhas, Dk Joseph Sempombe ametangaza kifo cha Kahitwa leo Mei 20, 2018, akisema chuo kitaendelea kutoa taarifa kuhusu tukio hilo.

Chanzo cha habari kimeeleza kuwa mwili wa mwanafunzi huyo ulikutwa ndani ya chumba chake namba 65 katika hosteli ya Kagera.

Imeelezwa polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo na mwili wa Kahitwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
 
Pamoja na uchungu wa kuzaa, uchungu wa kifo cha mtoto wake mchanga lakini Hamida Gwota alizuiwa kuondoka hospitali kwenda kumzika mwanaye hadi alipe deni la Sh631, 584 za matibabu ya mtoto aliyefariki dunia.

Hamida alitakiwa kulipa fedha hizo baada ya mwanaye wa siku nne aliyezaliwa utumbo ukiwa nje, kufariki dunia wakati akitibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Mei 12.
 
Kwa mujibu wa Sera ya Afya, matibabu ya mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano ni bure. Lakini Hamida hakupata huduma hiyo.

“Nilizuiwa kuchukua mwili wa mwanangu mpaka ndugu walipofanikiwa kukusanya Sh631,584 ili kulipia gharama za matibabu,” alisema Hamida katika mazungumzo na Mwananchi nyumbani kwake Ukonga jijini Dar es Salaam, juzi.
 
Watu wanaogopa kuibiwa bhana,halafu uzuri wa kuweka private hata mkiachana hakuna atakayejua zaidi yenu,sasa hii"kuzinduana"mkiachana tu tunajua maana mtabadili id na kukimbia jf[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
#protectyourlovedones#
Kabisaaa u nailed it my dear. Kwanza bora muelewane kabisa PM kwamba uhusiano huu uwe na mipaka ipi na ipi ili kuepusha bifu zisizo na maana,sio chit chat wala MMU au celebrity unakuta vijembe mwanzo mwisho uzi una topic nyingine mashost wamekalisha kikao kumsengenya fulan kuwakwapulia inahuuuuusuuu pyeeee uzinduzi my msabwax
 
Mwanangu alifariki Mei 12, lakini nilizuiwa kutoka. Ilibidi nilale wodini huku mwili wake ukiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti hadi fedha zilipopatikana ndipo nikakabidhiwa.”

Hamis Gwota, baba mzazi wa Hamida, alisema alipopata taarifa ya kifo cha mjukuu wake alienda kuomba aelekezwe hatua anazopaswa kufuata ili wakabidhiwe mwili.
 
Nilipouliza nikaambiwa kuna bili na lazima ilipwe ndipo watupatie. Binafsi nilishangaa kwa sababu siku zote nimekuwa namsikia waziri wa Afya anasema mtoto chini ya miaka mitano hutibiwa bure,” alisema Gwota.

Alisema ilibidi waitishe kikao cha ndugu ili kuchangishana hadi zilipopatikana fedha hizo.

“Kwa hiyo wakati tunachangishana fedha, mwanangu aliendelea kubaki wodini hadi siku ya pili tulipokabidhiwa mwili baada ya kukamilisha malipo yote.
 
Nilijisikia vibaya lakini sikuwa na namna nyingine zaidi ya kuhangaikia fedha hizo.”

Gwota alisema kama ndugu wasingechangishana, basi binti yake angeendelea kusota wodini.

Naye Hamida alisema awali alitegemea bima yake ya afya ya NHIF ingemwezesha kugharimia matibabu ya mwanaye aliyezaliwa akiwa anaumwa, lakini haikuwa hivyo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma cha MNH, Aminiel Aligaesha alisema kwa mujibu wa sera za hospitali hiyo mgonjwa yeyote aliyepewa rufaa akitokea hospitali binafsi, hupokewa na kutibiwa kama mgonjwa binafsi.
 
Back
Top Bottom