Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hzo jezi kweli ningekuwa nazo ungekuwa umeshanotice kitu hapa [emoji23][emoji23]

Nipo poa binti mpole, vipi huko, hali ya hewa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] safi kabisa,huku jua linaishilia hakuna dalili ya mvua
 
Licha ya vitamini E pia ndani ya parachichi kuna vitamini B6 na kuna madini ya chuma (Iron) kwa wingi na madini ya potassium, pamoja na vitamin B6 na E mlaji anaweza kuletawa nafuu sana kama alikuwa na matatizo ya stress, matatizo ya uzazi kama ugumba na jogoo kutopanda mtungi Nguvu za kiume pia tunda hili linasaidia (impotence) .
 
FAIDA ZA PARACHICHI
Licha ya binadamu kufaidika na virutubisho vya tunda hili kuna faida nyingi za parachichi kama vile majani ya mti wake pamoja na magamba, baadhi ya watu hutumia kutibu maradhi ya kuharisha.

Majani na magamba hayo hutibu pia tatizo la gesi tumboni, kutuliza kikohozi pamoja na matatizo ya ini na kusafisha njia ya mkojo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa dawa za mitishamba, dawa hii haifai kutumiwa na wanawake ambao wana mimba kwani wakitumia inaweza kusababisha kuharibika kwa ujauzito.
 
HEDHI
Hata hivyo, wataalamu wa tiba mbadala wanasema dawa hiyo inaweza kuwasaidia sana wanawake ambao wameshindwa kuona siku zao kwa wakati, na wakitumia vyema wanaweza kuanza kuona siku zao.

Aidha, tunda hili linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, kwani parachichi lina nyuzinyuzi “fiber” ambayo ni muhimu kukinga kuta za utumbo.

Watu wenye maradhi ya anaemia, diabetes, matatizo ya mfumo wa neva, matatizo ya mishipa ya moyo hasa wa artery wanashauriwa kula tunda hili mara nyingi.
 
Lakini pia tunda hili limethibitishwa na wataalamu kuwa linapunguza kwa kiwango kikubwa cholesterol kutoka kwenye damu hasa kwa watu wanene.

Tunda hili husaidia kulainisha ngozi na kuondoa mikunjo, hung`arisha na kulainisha nywele na kuzisaidia kukua pia kuziimarisha na kuzuia kukatikakatika.

Parachichi unaweza kulila kwa kulimenya au kwa kulisaga na kutengeneza juisi na kama nilivyoeleza hapo juu unaweza kuchanganya na matunda mengine kama tulivyoyataja na hutaharibu virutubisho vilivyomo badala yake utaongeza ubora wa juisi yako.
 
Watoto wadogo pia unaweza kuwapa tunda hili na wakafaidika na haya tuliyoyaandika.

Parachichi pia huweza kutumika kama siagi kwa kupaka kwenye mkate au kuchanganya na wali.

Haya wale wanaopenda ngozi zao za mwilini zisijikunje hata wakiwa watu wazima wadumu kula tunda hili kila siku katika maisha yao basi ngozi za mwili wao hazitajikunja hata usoni watakuwa kila siku vijana hata wakiwa wazee
 
Wanaume wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la kutokwa na vipele mara tu baada ya kunyoa ndevu zao.

Mbaya zaidi asilimia kubwa ya wanaume wamekuwa wakishindwa kujua nini cha kufanya ili kuondoa tatizo hilo ambalo pia huharibu muonekanano wa mhusika.
 
Hapa napenda kukueleza kuwa tunda la parachichi nalo huweza kuondoa tatizo hilo au kupunguza madhara kwa mtu mwenye shida hiyo.

Jambo la kufanya ni kupata tunda hili fresh kisha limenye na baadaye kulisaga halafu utalitumia mara tu baada ya kunyoa ndevu zako kwa kupaka rojorojo hilo la parachichi sehemu zote za kidevu yaani hii unaweza kuiita 'after shave ya asili'.
 
..
Screenshot_2018-05-20-17-19-57-1.jpg
 
Back
Top Bottom