Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3.Mkono wa mungu .

Hii ilikuwa kombe la dunia mwaka 1986 ambapo england walikutana na argentina katika hatua ya mtoano. Mnamo dakika ya 51 ya mchezo Maradona ambae alikuwa nyota wa argentina aliipatia argentina goli kupitia mkono ambapo kipa wa england peter shilton alipishana na mpira huo. Na mwenyewe maradona aliuita ni mkono wa mungu. lakini cha kushangaza zaidi wachezaji 5 waliounda kikosi cha england walilipigia kura goli hilo na kuwa goli ya karne kupitia tovuti ya FIFA.COM
Robo fainali hyo muingireza anakufa 2 goli bora kwangu ni lile anadribble mpira toka katikati ya uwanja akiwalamba chenga wachezaji wa england kama ya kwenda kummalizia golikipa peter shilton kabla ya kuweka mpira nyavuni.
 
katika fainali hizo kocha wa Brazil hakumuita pele katika chaguzi zake ila aliambiwa na rafiki zake pele kwamba kijana ni mchezaji mzuri na anaweza kuisaidia timu. Mechi yake ya kwanza alicheza dhidi ya sweden na katika mchezo huo alifunga hat -trick katika ushindi wa 5-2 na kuwa nyota wa mchezo na toka kumalizika kwa mechi alifunga karibia mechi zote alizocheza katika mashindano.
Katika mchezo huo alifunga goli moja maridadi ni moja kati ya magoli yangu bora zaidi kutoka kwa babu pele, alipokea mpira katika box akaukontro kwa kuweka kifuan maridadi kisha akampiga kanzu kiufundi beki wa sweden kisha akaachia kick kali iliyojaa moja kwa moja wavuni.
 
Back
Top Bottom