Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

DALILI:
Shambulio la ugonjwa huu likijitokeza uanza na kupotewa na fahamu na muda mfupi baadae mwili, miguu na mikono uanza kukakamaa na kurudisha kichwa nyuma, baada ya hayo miguu na mikono uanza kujitikisa.
Kushindwa kupumua na kutokwa na mapovu mdomoni
 
Macho kugeukia nyuma na kuonekana kwa sehemu nyeupe ya jicho
Shambulio huisha baada ya muda mfupi mara nyingi chini ya dakika tano
Baada ya shambulio hupitiwa na usingizi mzito kama takribani dakika 30 hadi saa nzima.
Akizinduka anaweza kushindwa hata kukutambua na akawa atamani kitu chochote kwa muda huo.
 
KINA NANI HUWAPATA ZAIDI DEGEDGE?
Degedege inaweza kumpata mtu yoyote wa umri wowote ijapokuwa mara nyingi inawatokea watoto wadogo walio na umri chini ya miaka mitano.Ndio maana wengine wanaita homa ya watoto/kitoto
 
NINI CHA KUFANYA MTU AKIPATWA NA DEGEDEGE?

Msaidie mgonjwa alale upande.
Ondoa vitu vyovyote (vigumu au vyenye ncha kali) vinavyoweza kumdhuru mgonjwa.
Weka kitu laini mfano nguo iliyokunjwa chini ya kichwa cha mgonjwa.
Usimpulizie hewa mdomoni; fanya hivyo iwapo hataweza kupumua baada ya degedege kukoma.
 
Fungua nguo au kitu chochote kilichoko kwenye shingo ambacho kinaweza kuathiri upumuaji.
Usijaribu kumzuia mgonjwa kwa kumkandamiza au kushika mikono na miguu
Kuwa mtulivu na hakikisha wale wote waliowazunguka wanakuwa watulivu.
Baki na mgonjwa hadi degedege litakapokoma lenyewe
Onesha upendo wakati anaporudiwa na fahamu
Iwapo ataonekana kuchanganyiwa, omba msaada.
 
MADHARA YATOKANAYO NA DEGEDEGE.
Mgonjwa mwenye degedege asipopata tiba sahihi kwa wakati anaweza kupatwa na madhara yafuatayo

Kupata tatizo la Kifafa.
Mtindio wa ubongo kwa watoto inaweza kupelekea ulewa duni katika masomo na hata mambo mengi akiwa nyumbani.
Ukuaji duni kwa mtoto hasa kama degedege ikiwa itamtokea mara kwa mara na hatimye motto atadumaa.
Kuwa na usikivu duni na uoni hafifu.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Huujui mpira kwa hiyo huta ni annoy
Halaf mnakuwaga mnatuhurumia tukifungwa hata mkitoa utani tunajua mna tu tease tuu

I will handle you well
mimi sitahitaji kujua kama najua mpira ama la ishu nikishajua mmefungwa akiii hutakaa karibu yangu nitakucheka hadi ukimbie na uendelee kununa[emoji23][emoji23][emoji23]
Huwezi niletea stress za mpira nyumbani mimi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…