Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MFAHAMU NYANI.

Nyani ni kiumbe mwenye ufanano wa mambo mengi sana na binadamu, pamoja na ufanano huo lakini ana tofauti sana na mwanadamu, iliyokubwa ni kwamba binadamu ana ufahamu timamu wa kuratibu na kujiongoza katika mambo mazuri na mabaya, wakati kwa viumbe wengine wote bahati hiyo hawana.
 
Ifahamike kwamba nyani ni miongoni mwa viumbe ambao hufanana sana na viumbe wengine wa jamii yake, kiasi kwamba viumbe hao nao huitwa nyani, wanyama ambao hufananishwa na nyani ni pamoja na sokwe, mbega, tumbiri na jamii zote za kima pamoja kuwa na majina yao hayo lakini binadamu awaonapo huwaita nyani.
 
Jike huwa mdogo kwa dume, urefu wake jike mkubwa huwa sm 60 sawa na rula mbili na dume huwa na sm 70, kwa uzito madume huwa zaidi pia hufikia mpaka kilo 60 na zaidi, jike hupevuka afikishapo miaka 5 mpaka 7, na hudumu na mimba kwa miezi 6, mpaka hapo atapozaa mtoto wake mmoja, nyani hawa huishi kwa miaka zaidi ya 25, chakula chao kikuu huwa nafaka na nyama, hivyo ni wanyama wa kundi la kati ambao hula mimea na nyama, chakula chochote anachokula mwanadamu nyani pia huweza kukitumia.
 
Katika kundi la nyama hupendelea samaki, kuku, sungura, panya, mbuzi, kondoo, upande wa nafaka hula karanga, mtama, mahindi, ulezi nk, pia matunda takribani yote tunayotumia nao hutumia mfano ndizi, tikiti, embe, nanasi nk.
 
Wawapo katika makazi yao huishi kwa familia, hutengeneza uongozi wao na uongozi huo hueshimiwa, ambapo watakuwepo walinzi, wawindaji, pamoja na viongozi wakuu wa Kitaifa ambao ndio hufanya maamuzi pindi linapotokea jambo la kuamriwa, viumbe hawa ni waumini wazuri wa demokrasia hufanya maamuzi kwa kukubaliana, na endapo miongoni mwao watakuwepo ambao wanapingana na maamuzi hayo basi jukumu lao huwa ni kuondoka katika utawala huo na kwenda kuanzisha makazi yao mapyaa.
 
Hata hivyo wapo ambao ni watukutu hususani madume hasa vijana, ambao na wao hujaribu mara kadhaa kutaka kufanya mapinduzi katika utawala unaokuwepo, yanapofanikiwa hushika dola, lakini yakishindwa cha mtema kuni hufahamu radha yake ikoje.
 
Nyani pia ni viumbe ambao wanaamini sana katika mitala, ni jambo la kawaida sana dume kumiliki majike zaidi ya watatu, mbali na mfumo wao huo pia ni viumbe ambao wanaamini sana katika mfumo dume, jike ndio huwa na hati miliki ya watoto hivyo anapopata majukumu ya kufanya kuliko ampeleke mwanaye kwa dume lake, huwa tayari amuachie mwanaye rafiki yake, jike la nyani katu haliwezi mkabidhi mwanaye kwa mke mwenzie kwani historia zao za uke wenza huanzia kwenye urafiki tuu, kwa mantiki hiyo wake wenzie wote huwa ni sehemu ya adui zake, endapo mtoto wake huyo atakuwa dume siku atayopevuka jike atapewa na dume ambalo ndio litakuwa linaongoza kaya hiyo na si vinginevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…