Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kalisi na gesi hiyo hupatikana katika chakula cha kome na katika maji. Ili kuiga ustadi wa kome, itatubidi kumeza mawe, kisha tuyachanganye mwilini mwetu, na kuyatoa yakiwa vifaa vya ujenzi vilivyo tayari kutumiwa kujenga kuta na madari! Lakini kitu kinachowasisimua sana watafiti si koa lenyewe; bali ni mguu wa kome.
 
GUNDI YA KOME INAYONATA SANA


Hebu jaribu kumwondoa kome kutoka kwenye mwamba. Utagundua kwamba yeye hunata kabisa mwambani. Ni lazima kome afanye hivyo ili akinze mawimbi yenye nguvu ya bahari au mashambulizi ya ndege wa baharini mwenye njaa anayetumia mdomo wake uliochongoka.

Yeye huwezaje kujishikilia kwa nguvu hivyo?
 
View attachment 788396
 
GUNDI YA KOME INAYONATA SANA


Hebu jaribu kumwondoa kome kutoka kwenye mwamba. Utagundua kwamba yeye hunata kabisa mwambani. Ni lazima kome afanye hivyo ili akinze mawimbi yenye nguvu ya bahari au mashambulizi ya ndege wa baharini mwenye njaa anayetumia mdomo wake uliochongoka.

Yeye huwezaje kujishikilia kwa nguvu hivyo?
 
Chaza anapochagua maskani yake, yeye huchomoza mguu wake wenye umbo la ulimi nje ya koa na kuufinya mahala pagumu, ambapo Tezi_Fulani_Maalumu hufanyiza na kutoa umajimaji wenye protini kupitia kijia kilicho kwenye mguu huo.
Umajimaji huo hukauka upesi na kuwa uzi mwembamba unaonyumbulika wenye urefu wa sentimeta mbili hivi, Kisha sehemu ndogo iliyo kwenye ncha ya uzi huo hutoa utomvu mdogo wa gundi kwa nguvu.
 
Kome huinua mguu wake, na hatua ya kwanza ya kujishikamanisha humalizika. Nyuzi hizo zilizowekwa kwa ustadi huungana na kuwa kitita kinachoitwa BYSSUS. Kitita hicho humfunga kome imara kwenye maskani yake mpya kama vile kamba za kukazia hema zinavyolikaza hema liwe imara. Kazi hiyo huchukua dakika tatu au nne tu.
 
Madaktari-wapasuaji wangependa gundi inayonata kabisa kwa minajili ya kuunganisha mifupa iliyovunjika na kufunga majeraha.

Madaktari wa meno wangeitumia kuziba mashimo kwenye meno na kurekebisha meno yaliyovunjika. Gundi hiyo ingetumiwa kufanya mambo mengi sana.
 
Hata hivyo, wanasayansi hawafikirii kuwatumia kome ili kutengeneza gundi hiyo inayonata sana, Mfano Ili kutengeneza gramu moja tu ya gundi hiyo, kome 10,000 watahitajiwa, Kwahiyo iwapo njia hiyo ingetumiwa ili kutosheleza mahitaji ya ulimwengu ya gundi, kome wote wangemalizika, na tayari jamii nyingi zimo hatarini.
 
Back
Top Bottom