Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Badala yake, watafiti wa Marekani wametenganisha na kutokeza chembe nyingine za urithi ili kupata protini tano za kome zinazofanyiza gundi. Hivi karibuni watazitokeza kwa wingi katika maabara ili ziweze kujaribiwa viwandani.
Pia, wanasayansi wa Uingereza wanafanya utafiti kuhusu mojawapo ya protini hizo za gundi. Hata hivyo, bado kome amewashinda. Ni kome tu ajuaye mchanganyiko sahihi wa protini unaoweza kushikamanisha vitu mbalimbali. Frank Roberto, mwanabiolojia wa molekuli, aliuliza hivi kwa kustaajabishwa: “Je, mtaweza kweli kuiga jambo hilo?”
 
Mfagiaji

Kome hula kwa kuchuja maji. Katika jamii nyingi za kome, kila kome huingiza lita kadhaa za maji mwilini kila siku na chakula, oksijeni na vilevile vichafuzi kama bakteria zinazodhuru na kemikali zenye sumu huchujwa. Kome husafisha maji vizuri sana kwa kutumia uwezo huo.
 
Pia, wao hutumiwa kujua kimbele iwapo maji yamechafuliwa. Kwa mfano, mamia ya kome wameingizwa baharini karibu na eneo la Ekofisk lenye visima vya mafuta, karibu na pwani ya Norway. Kila baada ya miezi kadhaa, wanasayansi huwaondoa kwenye maskani yao na kupima kiasi cha uchafu ulio ndani ya magamba yao ili watambue iwapo kemikali zinazoingia baharini zinawadhuru viumbe wanaoishi humo.
 
Tangu mwaka wa 1986, kome na chaza wametumiwa katika Mradi wa Mussel Watch kwenye sehemu za pwani na za bara katika Amerika Kaskazini. Watafiti hujua iwapo kuna mabadiliko yoyote katika ubora wa maji kwa kuchunguza chaza hao kila mwaka kuona kama wamemeza kemikali. Chaza hao wana faida kubwa kama nini!
 
Mara nyingi, jamii moja ya kome inayopatikana kwenye maji yasiyo na chumvi huonwa kuwa kiumbe mharibifu. Kome huyo mwenye milia huitwa kome aina ya zebra.(pichani juu)

Kome huyo mdogo sana hupatikana hasa mashariki mwa Ulaya. Yamkini aliingizwa Amerika Kaskazini kiaksidenti katikati ya miaka ya 1980 wakati meli moja iliyokuwa ikivuka bahari ya Atlantiki ilipomwaga maji yanayofanya meli iwe thabiti. Tofauti na kome wengine, idadi ya kome aina ya zebra imeongezeka sana katika yale Maziwa Makubwa na milango-bahari iliyo kando yake na kusababisha hasara ya mamilioni ya dola kwa kuziba mabomba ya maji na kufanyiza magamba kwenye mashua, magati, na madaraja. Pia, kome huyo amepunguza idadi ya jamii nyingine kadhaa za kome zinazopatikana hasa katika eneo hilo.
 
Hata hivyo, kome hao wana faida fulani. Kwa kuwa kome aina ya zebra ndio walaji bora wa kuchuja maji, wao husafisha maji meusi ya ziwa haraka kwa kumeza mimea ya mwani inayoelea. Kisha, mimea ya kijani ambayo humea majini inaweza kunawiri tena na kuwaandalia makao viumbe wengine wanaoishi ziwani. Kwa sasa, wanasayansi wanachunguza iwapo wanaweza kutumia uwezo wa kome hao wa kuchuja maji ili kuondoa bakteria zinazodhuru kutoka kwenye mabwawa ya maji ya umma na hata kuondoa taka kutoka kwenye viwanda vya kusafishia maji machafu.
 
Hamna picha google tu utaiona
 
STADI NYINGINE.

Je, ulijua kwamba kome fulani wanaopatikana kwenye maji yasiyo na chumvi hutengeneza lulu za asili, nyingine za thamani kubwa sana? Iwapo umewahi kuvaa vito vilivyofunikwa kwa lulumizi au umetumia vifungo vya lulu, huenda pia vilitengenezwa kutoka kwa kome. Lulumizi zinazong’aa zenye rangi ya upinde wa mvua, hufanyizwa kutokana na tabaka la ndani la koa za kome, na hutumiwa mara nyingi katika biashara ya kutengeneza lulu. Punje ndogo sana ya lulumizi, iliyokatwa kutoka kwenye koa la kome, huingizwa ndani ya chaza. Chaza anapowashwa na punje hiyo, yeye huanza kuifunika kwa lulumizi. Hatimaye, yeye hutokeza lulu.
 
Bila shaka, sisi hula kome fulani wa baharini pia! Kwa karne nyingi, watu wamefurahia kula nyama laini ya kome yenye lishe, inapopikwa kwa njia mbalimbali. Katika nyumba za Wafaransa, huenda ukala moules marinière, yaani kome aliyepikwa kwa kuchemshwa katika mchuzi wenye mvinyo na aina fulani ya vitunguu. Wahispania hupendelea kuwapika kwa kutumia viungo vingi. Chakula hicho huitwa paella. Nao Wabelgiji huwaandaa wakiwa moto katika sufuria kubwa na kuwala kwa chipsi.
 
Bila shaka, sisi hula kome fulani wa baharini pia! Kwa karne nyingi, watu wamefurahia kula nyama laini ya kome yenye lishe, inapopikwa kwa njia mbalimbali. Katika nyumba za Wafaransa, huenda ukala moules marinière, yaani kome aliyepikwa kwa kuchemshwa katika mchuzi wenye mvinyo na aina fulani ya vitunguu. Wahispania hupendelea kuwapika kwa kutumia viungo vingi. Chakula hicho huitwa paella. Nao Wabelgiji huwaandaa wakiwa moto katika sufuria kubwa na kuwala kwa chipsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…