Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Utafiti huo umegunduliwa na Watafiti wa Ujerumani ambao walichunguza kwa kina watumiaji au walaji wa chakula chenye mafuta mengi kwa wakati mmoja ikiwemo hamburger, chips na pizza unaweza kuathiri umetaboli wa mwili, na kusababisha ugonjwa wa maini yenye mafuta na ugonjwa wa kisukari.
 
Kituo cha utafiti cha ugonjwa wa kisukari cha Ujerumani kimesema, wamewashirikisha wanaume wembamba wenye afya nzuri kwenye utafiti, na kuwapatia kikombe chenye mafuta ya zaituni au kikombe cha maji bila mpangilio. Mafuta ndani ya kinywaji kile ni sawa na hamburger mbili za nguruwe pamoja na chipsi au pizza mbili.
 
Watafiti hao walitumia njia ya MRI na kugundua kuwa, ulaji wa mafuta mengi kwa wakati mmoja unaweza kupunguza mchango wa insulin, na kusababisha ongezeko la kuzuia insulin na kiwango cha mafuta kwenye maini, huku ukileta athari kwrnyr umetaboli wa maini ambayo inafanana na athari zinazotokana na ugonjwa wa kisukari wa aina II au maradhi ya ini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…