Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

VUTA PICHA: “unaathirika kisaikolojia kwanini..?” kwa kuwa kunguni wanatabia ya kunata kwenye pindo za nguo, na pindi unapoivaa nao huwepo, hivyo pindi unapotembea nao na kwenda mazingira tofauti, nao huambua na kuanza kuhama au kutoka sehemu waliyokuwepo na kuzurura ili kutafuta sehemu nyingine iliyosalama zaidi kwao kujificha.
Watu walioumwa na kunguni wanaweza kupoteza usingizi, kuaibika, na hata kufikiri kwamba kunguni amewauma muda mrefu baada ya wadudu hao kutoweka, Jarida moja nchini Sierra Leone linasema kuwa kunguni “ni wasumbufu sana na wanawakosesha watu usingizi” na linaonya kuhusu “aibu inayohusianishwa na kunguni.”
 
KUWADHIBITI KUNGUNI
Kunguni wanaweza kumsumbua mtu yeyote, Ni rahisi kuwadhibiti ukitambua mapema kwamba wapo, Kwa hiyo, jifunze kutambua ishara za kwamba wapo nyumbani na unaposafiri, Chunguza fanicha zako na vitu vingine vya mbao pamoja na mizigo, uone ikiwa kuna mayai madogo yanayofanana na mbegu ndogo nyeusi au alama za damu.
 
Usiruhusu kunguni wawe na sehemu nyingi za kujificha vyumbani mwako, Ziba nyufa zote ukutani na kwenye viunzi vya milango, Ingawa kunguni hawaletwi moja kwa moja na uchafu, lakini ndio kivutio chao kikubwa, hivyo itakuwa rahisi zaidi kwako kuwatambua na kuwadhibiti ikiwa unasafisha nyumba yako mara kwa mara sehemu zile zisizofikika kirahisi kama uvunguni mwa kitanda, kwenye kona nza makabati, chaga nk. Pia, epuka kuacha fenicha zako zikirundikana sehemu moja kwa muda mrfu, badilisha mkao wa fenicha zako mara kwa mara na kupunguza vitu vilivyorundamana / kurundikana visivyotumika maeeo hayo.
 
MWISHO: KUNGUNI WANAPOVAMIA NYUMBA YAKO
Ukipata kunguni nyumbani au hotelini, huenda ukawa na wasiwasi au hata ukaaibika. Mfano nchini Uingereza , Japhet na mke wake waliumwa na kunguni walipokuwa likizoni. Japhet anasema: “Tuliaibika sana. Tulijiuliza tutawaambia nini watu wa familia na marafiki tutakapofika nyumbani? Je, wakati wowote wanapojikuna au kupatwa na mwasho wa ngozi wangejiambia ni kwa sababu walitutembelea?”
 
Hata ingawa ni kawaida kuwa na maoni kama hayo, usiache aibu ikuzuie kutafuta msaada, Wizara ya Afya ya Mwili na Akili ya New York City iliwahi kutoa uhakikisho huu: “Ni vigumu, lakini inawezekana kuwaangamiza kunguni, endapo Ukitafuta mbinu za kupambana nao.”
Kanza Chunguza uone kama kuna kunguni, pili chukua hatua za kuwazuia wasijifiche nyumbani kwako na kuondoka.
 
Hata hivyo, usifikiri kwamba ni rahisi kuwamaliza kunguni, Kunguni wakivamia nyumba yako, unaweza kupata msaada kutoka kwa mtaalamu wa kuwadhibiti wadudu hao wasumbufu.
Ingawa kemikali na sumu zilizotajwa awali hazitumiwi tena, lakini wataalamu hao hutumia mbinu kadhaa zinazofaa ili kuwaangamiza kunguni, ikiwemo watu wengine hutumia majivu, au majani ya maharagwe kuwanasa nk.
 
Dini M. Miller, mtaalamu wa wadudu anasema hivi pia: “Kuwadhibiti kunguni kunahitaji ushirikiano mkubwa sana kati ya wakaaji wa nyumba, wamiliki wa nyumba yenyewe, na kampuni ya kuwadhibiti wadudu wasumbufu kama hao.” Kwa kufuata mwelekezo wa mtaalamu na kuchukua tahadhari zinazohitajika, unaweza kutimiza sehemu yako na ‘kutowaacha kunguni wakuume’!
Wataalamu wa wadudu wanasema kwamba kunguni hula damu ya wanadamu na wanyama wengine kutia ndani wanyama-vipenzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…