Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 183,580
- 1,105,911
Duuu, yule kibopa wakati ule akisurubika
HahahahahahaBujumbura, Burundi. Punda 10 walionunuliwa na Ufaransa kutoka Tanzania na wakatolewa kama zawadi katika kiijiji kimoja hapa nchini wameibua mjadala hadi kufikia kusema zawadi hiyo ni ‘matusi kwa taifa’.
Haraka Wizara ya Kilimo ikaamuru kuwaweka chini ya karantini punda hao hali iliyozua mjadala kuhusu ujumbe uliomo katika zawadi hiyo.
Punda hao, walionunuliwa kutoka Tanzania kutokana na fedha za mfuko wa misaada wa Ufaransa walitolewa kama zawadi kwa wakazi wa kijiji cha mkoa wa Gitega ikiwa ni mradi uliobuniwa na shirika lisilo la kiserikali kuwasaidia wanawake na watoto kusafirisha mazao ya kilimo, maji, kuni na mizigo mingine.
Toa kama unavyopewa
[emoji3] [emoji3] [emoji3] zawadi ni zawadiMshauri wa rais ameuelezea mradi huo kuwa sawa na “matusi kwa taifa.”
Msemaji wa Rais wa Seneti, Gabby Bugaga aliandika katika Twitter akisema Ufaransa “inatuchukulia sisi kama punda”.
“Kuweni wakweli, je, punda anachukuliwa kuwa alama ya ubora au ni kasoro?” Aliandika.
[emoji3] [emoji3] [emoji3]Burundi yakamata punda wote
Jumapili, Waziri wa Kilimo, Deo Guide Rurema alimwagiza kiongozi wa serikali katika eneo hilo kusaidia haraka kuondolewa punda wote ambao wameshagawiwa bila kujali mchakato wa kiufundi uliofikiwa katika kugawa wanyama hao kutoka nje.
Alhamisi iliyopita, siku ambayo mradi huo ulizinduliwa, Balozi wa Ufaransa Laurent Delahousse alipongeza “uzinduzi wa Land Cruiser aina ya wanyama Burundi”.
Baada ya kuibuka utata huo balozi huyo alisema kwa uelewa wake ‘taratibu zote zilifuatwa.’
Ubelgiji imewahi kuzindua miradi kama hiyo katika mkoa wa Ryigi lakini haikuwa na tatizo lolote.