Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hahahaha ukibisha hapa basi wewe unaweza mshinda mtu wa kigoma kwa ubishi

KUTANDIKA KITANDA

kama ulikuwa hufahamu asilimia 21 ya watu duniani huamka asubuhi pasipo kutandika vitanda vyao.
Huwez nidanganya kirahisi hvo Numby
IMG_20180528_075800.jpg
 
Kuiangusha Goguryeo ilibidi kuwe na Kolabo zito baina ya Ufalme wa Uchina (Tang-Dynasty) na Ufalme wa SILLA. Tena walijaribu zaidi ya mara tatu hivi ndiyo wakafanikiwa. Ndiyo maana hata baada ya Goguryeo kuangua Ufalme ule wa Kaskazini uliomrithi (Goryeo Empire) ulikiwa na nguvu sanaa kijeshi japo ulikuwa mdogo.

NB: Ukitaka kufahamu nguvu ya Goguryeo lazima ujiulize kwamba ni Ufalme upi wa Mashariki ya mbali umewahi kudumu kwa zaidi ya miaka 700 mfululizo bila kuvamiwa ?? Hata Uchina haukuwa hivyo. Lakinj baharti mbaya kilichowaangusha ni mpasuko wa kisiasa na kikabila uliokuwepo ndani ya nchi......Tang na Silla walithubutu kupigana nao baada ya kugundua nchi iko kwenye vita vya wao kwa wao. Lakini hivi hivi wangetoka kapaaaa maana jamaa walikuwa siyo mchezooo.
madaraka ni ugonjwa hatari sana kuliko ugonjwa wa kisukari ambao hukufanya ukatwe kila kiungo kilichoathirika zaidi.
na nchi yoyote itakayoendeshwa bila ya kuwepo kwa maridhiano kati ya pande zinazokinzana kimtazamo haiwezi kufanikwa kwa jambo lolote na hilo ndio liliifanya goguryeo ijikute kwenye wakati mgumu.
Yon_Kaesomun.gif

  • kulikuwa na upande ambao ulitaka goguryeo ianzishe mahusiano ya kirafiki na Tang kama alivyofanya kim chunchu wa SILLA (pro tang) ili kuondoa minyukano ya kila mara kati ya mataifa hayo mawili, upande huo uliongozwa na koo zenye nguvu ambao waliangalia zaidi maslahi yao binafsi kwa sababu waliamini goguryeo na Tang wakiwa marafiki basi mahusiano ya kibiashara yatakuwa makubwa zaidi, kama tunavyofahamu china ndio kituo cha biashara duniani.
  • upande wa pili ni wale ambao walipinga goguryeo wasiwe na urafiki wa karibu na Tang kwa sababu waliamini kuikaribisha TANG ni hatari zaidi kwa maslahi ya goguryeo kuendelea kuwepo kwa sababu tawala zote za china ziliinyemelea goguryeo kwenye vita nyingi lakini goguryeo ilisimama imara bila ya msaada wowote, upande huu uliongozwa na general yeon gae somun.

baada ya sintofahamu ya muda mrefu na kila upande kudhamiria kusambaratishana ndipo siku moja ya mwaka 642 shujaa yeon gaesomun na wafuasi wake walifanya sherehe kwa ajili ya kumpongeza yeon gaesomun kuchaguliwa kuwa governor wa mashariki. kwenye sherehe hizo aliwaalika wapinzani wake takribani 100 na ndipo akawaua wote kwenye sherehe hiyo na baadae kuelekea ikulu ambako alimuua mfalme yeongnyu.
baadae yeon gae somun akamchagua mpwa wa mfalme ambaye ni mfalme bojang awe mfalme wa 28 wa goguryeo ambaye ndie mtawala wa mwisho.
yeon gae somun akajipa cheo cha mangniji (superior commander) hivyo basi goguryeo ikawa inaendeshwa kwa akili ya mtu mmoja(de facto control) na mfalme alibaki kuwa kama mbwa koko.
uwepo wa yeon gaesomun kama mkuu wa nchi kulizidi kuchochea mgogoro wa Tang na goguryeo na ndipo lishimin akajaribu kuivamia goguryeo lakini mara zote alishindwa vibaya sana.
moja kati ya ushindi mkubwa wa yeon gaesomun ni kwenye vita ya sasu river mnamo 662 baada ya kumdhibiti general Pang Xiaotai na jeshi lake, kwenye vita hiyo alimuua pang xiaotai na pia aliwachinja watoto wake 13.
vita za mara kwa mara zilipelekea uchumi wa goguryeo kudorora na miaka mitatu baadae yeon gae somun alifariki dunia.
kifo cha yeon gaesomun kilichochea anguko la goguryeo kwa sababu watoto wake waliwaniana madaraka na kusahau dhamira na lengo kuu la baba yao kuwa mangniji.
yeon namseng akaamua kuomba msaada kwa Tang kwa kuamini ya kwamba Tang watamsaidia kumuondoa madarakani mdogo wake ili awe mangniji kwa mara ya pili na mdogo wake mwengine akaamua kuomba msaada kwa SILLA ili awe mangniji.
kwa hivyo TANG na SILLA waliitumia nafasi hiyo kuuangusha utawala wa goguryeo.
udikteta ni mbaya sana na nimeanza kuona dalili ya nchi moja hapa afrika mashariki kuongozwa na akili ya mtu mmoja peke yake.
anajua uchumi peke yake
anajua siasa peke yake
anajua biashara peke yake
anajua maswala ya uwezekezaji peke yake
anajua maswala ya diplomasia peke yake
anaamua peke yake kutoa tenda
anaamua peke yake eneo la kujengwa uwanja wa ndege
mwisho wa siku ataamua peke yake ni andishi gani Malcom Lumumba awasilishe jamiiforums
ㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋㅋ
 
Back
Top Bottom