Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

439637272_230481.jpg
 
Wema ashindwa kufika mahakamani, inadaiwa yupo India kwa matibabu

Mwigizai Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya mapema wiki hii ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kujitetea katika kesi yake kwa sababu amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.

Mama yake, Mariam Sepetu ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa serikali, Constantine Kakula kuhoji kwa nini Wema hakufika mahakamani.
 
Dk Bashiru Ali aukwaa Ukatibu Mkuu CCM

Baada ya Abdulrahman Kinana kujiuzulu, Dk Bashiru Ally ndiye aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu Mpya wa CCM ambapo alipendekezwa na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, Ikulu jijini DSM.

Hii ni baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kinana kuomba kujiuzulu na kukubaliwa na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa.

Dk Bashiru Ally alikuwa Mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na Rais Magufuli kufanya Uhakiki wa mali za Chama cha Mapinduzi CCM.
 
Mugabe awekwa mtegoni

Aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe kwa mara ya pili ameshindwa kufika mbele ya Kamati ya Uchunguzi ya Mapato ya Almasi ya Bunge la nchi hiyo.

Rais huyo aliyeongoza kwa muda mrefu hadi alipotolewa madarakani Novemba mwaka 2017, ametakiwa kufika Bungeni hapo tarehe June 11, 2018 bila kukosa.
 
Mangwair atimiza miaka mitano tangu afariki

Mei 28, 2013 mkali wa freestyle, Albert Mangwair alifariki dunia akiwa Johannesburg nchini Afrika na kuacha pengo kubwa katika muziki wa Bongo Fleva

Marehemu Mangwair alianza kazi ya muziki mwaka 2003 na kuachia ngoma yake ya kwanza “Ghetto Langu” ambayo ilimfungulia milango ya maisha yake katika muziki na kumpatia umaarufu.

Nyimbo zake nyingine maarufu ni Sikiliza, She Got Gwan, Mikasi, A.k.a Mimi, Napokea Simu, Mademu Zangu na CNN.
 
Back
Top Bottom