Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nikiwa nimekaa nje baada ya kumaliza uchunguzi wangu, namshuhudia mlemavu mmoja akirejea mnamo saa 1:00. Huyu ni mlemavu wa miguu hivyo anatembea kwa kutumia mikono. Lakini katika kazi, anatumia baiskeli akisukumwa na kijana.

Baadaye wakaanza kumiminika mmoja baada ya mwingine. Kila anayefika, humwaga kitandani fedha alizopata na kuzihesabu na wakati huo, hufunga mlango kuzuia watu kuingia.

Saa 4:00 usiku anaingia mwanamke mnene kuwaletea chakula; wali na maharage. Muda huo, walemavu hao hutengewa chakula jirani na choo.
 
Wanaowasukuma hutoka nje kuchukua chakula kilichowekwa kwenye mifuko ya rangi nyeusi na kuingia nacho vyumbani kwa ajili ya kula.

Aina ya walemavu

Ndani ya nyumba hii ya wageni kuna walemavu 13 na kati ya hao watatu ni wa kike. Wawili wana ulemavu wa kichwa kikubwa, pia yuko mlemavu ambaye amepooza mikono na miguu, ambaye jina lake ni Ndebhile ambaye kwa kipindi nilichokuwapo hapo amekuwa akitengewa chakula peke yake jirani na mfereji wa maji machafu.

Pia, wapo ambao miguu yao imepinda na wanatembea kwa kutumia mikono, mmojawao akiwa ni Ndebhile.

Ni miongoni mwa walemavu wakorofi na wagomvi, muda wote anakuwa na hasira na anapotembea hataki mtu akatize mbele yake kwa kuwa hutembea kwa kasi.
 
Mlemavu huyu anaongea vizuri kuliko walemavu wengine ambao baadhi hawawezi kuongea na wapo ambao wanaongea kwa tabu.

Kati ya hao 13, ni wawili tu ambao wana akili timamu na wanaojitambua, yaani Pili na Iyobhe au Dorcas ambaye nilimkuta akiwa amebebwa eneo la Gerezani na mama Juma.

Mama Juma ana mtoto mmoja wa kiume na Dorcas hana mtoto. Walemavu hawa ndiyo wenye uwezo hata wa kuzungumza na kueleza jambo lolote wanalolijua. Walemavu wengine hawajitambui na wala hawajui chochote.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Mawazo yanakimbia mbali sana hadi kwenye kifo hataru sana.

Ila nimeshare naamini kabisa nilivyoshea nime attempt kuli solve tatizo. Sababu nawewe ukivyonambia kuwa unali face kidogo imenipa ahuheni.

Thank you.
Kila tatizo lina pacha wake. Unaweza jiona upo alone kwenye mateso kumbe wengi tunateseka sema tu hatuna ujasiri wa kuongelea suala hilo hadharani
 
Katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuna changamoto ya muda kwa wafanyakazi hususani wanawake.

Changamoto ya muda inatokana na kuwapo kwa muda maalumu wa kufuturu (kula) na chakula maalumu (futari).

Kutokana na changamoto hiyo leo ninakuletea futari mbili ambazo unaweza kuziandaa kwa muda mfupi.

Futari hizo ni pamoja na ndizi mbivu na viazi mbatata.
 
Futari ya ndizi mbivu

Mahitaji

Ndizi mbivu sita

Nazi pakiti moja

Sukari kiasi

Hiliki ya kutosha



Jinsi ya kutayarisha

Menya ndizi kisha toa moyo wa kati kati, zikate kate kulingana na unavyotaka, zipange ndani ya sufuria.

Weka maji kiasi kulingana na wingi na ugumu wa ndizi, zichemke kidogo zikikaribia kuiva na kabla maji hayajakauka kabisa weka tui la nazi, mimina hiliki na sukari ziache zichemke hadi tui libaki kidogo, zitakuwa tayari kwa kuliwa.
 
Futari ya viazi mbatata

Mahitaji

Viazi mbatata kulingana na ukubwa wa familia ua watakaokula.

Nyanya

Vitunguu

Pili pili hoho

Karoti

Mafuta ya kupikia

Maji safi

Chumvi

Pili pili mtama



Maandalizi



Menya viazi, unaweza kuvikata au kuviacha vizima kulingana na unavyopenda.

Vioshe vizuri kwa maji safi.

Tayarisha nyanya, vitunguu, hoho na karoti

Bandika sufuria ya kupikia jikoni, weka mafuta ya uto, yakichemka weka vitunguu maji, vikiiva kiasi weka vitunguu saumu, kisha acha viive hadi viwe na rangi ya hudhurungi (brown).

Weka viazi mbatata kwenye mchanganyiko wa vitunguu koroga kwa muda na uviache kwa muda wa dakika 10 hadi 15 hadi vikaukie mafuta kisha weka nyanya hakikisha ukiweka nyanya moto uwe wa kutosha ili ziive.

Funika kwa dakika tano, geuza kisha weka hoho na karoti kwa pamoja kisha funika, hapa unaweza kupunguza moto baada ya dakika mbili au tatu geuza na hakikisha vimechanganyika na vimebaki na mchuzi mzito kisha viipue tayari kwa kuliwa.
 
Baada ya kupata taarifa za kutosha kuhusu maisha na maeneo wanayotoka walemavu 12 kati ya 13 wanaoishi kwenye ile nyumba ya wageni, niliamua kusafiri hadi mkoani Shinyanga.

Baada ya kuulizia, nilifika kitongoji cha Mondo, takriban kilomita 80 kutoka Shinyanga mjini ambako ni nyumbani kwa Pili Iyobhe.

Usafiri rahisi wa kufika katika kijiji hiki ni bodaboda na baiskeli pekee, kwa maana nyingine si rahisi kufika na gari.
 
Wakazi wa mjini Shinyanga wanakijua kijiji hicho kwa mauaji ya wanawake, ambao huviziwa wakati wanapokwenda kuchota maji au kusanya kuni, hivyo wageni hutahadharishwa.

“Unapokwenda huko unatakiwa uwe makini sana. Si sehemu salama kihivyo. Kwanza uendako ni mapori nyumba moja hapa na nyingine kule. Sisi wenyewe hatuendi huko mpaka kuwe na ziara ya kiongozi,” anasema mkazi mmoja wa mjini Shinyanga baada ya kumueleza kuwa naelekea katika kijiji hicho.
 
Barabara ya kuelekea kitongoji hiki imezungukwa na mashamba ya mpunga, mito na mapori makubwa, hakukuwa na barabara maalumu ya kupita bodaboda, tulilazimika kukatiza mbunga na wakati mwingine tulipotea njia na kutumia muda mwingi kutembea kwa miguu.

Kutokana na njia tulizokuwa tukipita kujaa maji na matope mengi, tulilazimika kuvua viatu na nguo ili kuyavuka.

Tofauti na vijiji vingine, ukitembea kilomita chache utakutana na nyumba za ibada, shule, vituo vya afya lakini kwa Shatimba hali iko tofauti kidogo.
 
Kwa safari yangu wakati wa kwenda na kurudi nilibahatika kuona kanisa moja tu linalomilikiwa na kaka yake Pili ambalo pia lipo umbali wa kilomita tano kutoka nyumbani kwa akina Pili.

Sikuweza kuona kituo cha afya wala shule ingawa niliona wanafunzi wachache wakitembea na wengine wakiwa na baiskeli nyakati za jioni, hali iliyonifanya niamini kuwa walikuwa wakitokea shule iliyo mbali na eneo hilo.

Ndivyo ilivyokuwa. Katika mazungumzo yangu na wenyeji nilielezwa kuwa shule iko kilomita sita kutoka kijijini hapo. Hata hivyo, wanafunzi wengi wanashindwa kwenda, hasa wa shule ya msingi kutokana na mito kujaa maji.
 
Futari ya ndizi mbivu

Mahitaji

Ndizi mbivu sita

Nazi pakiti moja

Sukari kiasi

Hiliki ya kutosha



Jinsi ya kutayarisha

Menya ndizi kisha toa moyo wa kati kati, zikate kate kulingana na unavyotaka, zipange ndani ya sufuria.

Weka maji kiasi kulingana na wingi na ugumu wa ndizi, zichemke kidogo zikikaribia kuiva na kabla maji hayajakauka kabisa weka tui la nazi, mimina hiliki na sukari ziache zichemke hadi tui libaki kidogo, zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Nitajaribu.
 
Kitu kingine ambacho si cha kawaida ni kijiji hicho kuwa na wazee wengi wanaume kuliko vijana na wanawake. Mara nyingi njiani tulikutana na wazee wakitembea pamoja wawili au watatu. Majumbani walikuwa kwenye vikundi wakicheza karata na kuongea.

Pia nilishuhudia vijana wadogo ambao kwa umri wao wanatakiwa kuwa shuleni, wakiwa wanachunga ng’ombe. Wanakijiji wengi wanajishughulisha na ufugaji, lakini pia wenyeji wa eneo hili wanasema ili uheshimike lazima uwe na ng’ombe wengi.

Wanawake wachache niliobahatika kuwaona, walikuwa katika shughuli za kilimo, kutafuta kuni na kuchota maji.
 
Nyumbani kwa akina Pili

Baada ya kuwasili kijiji cha Shatimba, nilianza kuulizia nyumbani kwa wazazi wa Pili kwa kufuata maelekezo yake wakati tulipoongea jijini Dar es Salaam kwenye nyumba ya kulala wageni walikopangiwa.

Pili aliniambia nikifika kijiji cha Shatimba niulizie kwa Mzee Iyobhe au kwa Mwanakakongo, jina ambalo alisema ni maarufu kijijini hapo.

Nilipata wakati mgumu kutokana na uchache wa watu na nyumba kuwa mbalimbali. Wakati tunaanza kuingia kijijini haikuwa rahisi kumpata mtu wa kumuulizia kwa kuwa hatukukutana na wenyeji kwa kuwa eneo kubwa ni pori.
 
Dereva wa bodaboda ambaye pia alionekana kuwa mwenyeji kidogo wa kijiji hiki, akanitaka tuendelee na safari tutafute sehemu ambayo nyumba zimejikusanya.

Tulitembea kwa mwendo wa nusu saa na kukutana na kijana ambaye nilihisi ana umri wa miaka 17 akiwa amebeba matunda ambayo sikuweza kuyatambua na kutugawia.

Baada ya dereva kumuulizia Mzee Iyobhe, kijana huyo alijibu kuwa hamfahamu na kutuelekeza kwenda katikati ya kijiji.
 
Back
Top Bottom